1 John 2:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata hivyo, amri hii ninayowaandikieni ni amri mpya, na ukweli wake unaonekana ndani ya Kristo na ndani yenu pia. Maana giza linatoweka, na mwanga wa kweli umekwisha anza kuangaza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini nawaandikia amri mpya, yaani lile neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu, kwa sababu giza linapita na ile nuru ya kweli tayari inang’aa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena nawaandikia amri mpya, neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu; kwa kuwa giza linapita na ile nuru ya kweli imekwisha kung'aa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini kile ninachokiandika pia ni amri mpya. Ni kweli; Mnaweza kuiona kweli ndani ya Yesu na ndani yenu ninyi wenyewe. Giza linatoweka, na nuru ya kweli tayari inang'aa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hata hivyo, amri hii ninayowaandikieni ni amri mpya, na ukweli wake unaonekana ndani ya Kristo na ndani yenu pia. Maana giza linatoweka, na mwanga wa ukweli umekwisha anza kuangaza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata hivyo, amri hii ninayowaandikieni ni amri mpya, na ukweli wake unaonekana ndani ya Kristo na ndani yenu pia. Maana giza linatoweka, na mwanga wa kweli umekwisha anza kuangaza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ninawaandikia amri mpya, yaani, lile neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu, kwa sababu giza linapita na ile nuru ya kweli tayari inang'aa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini nawaandikia amri mpya, yaani, lile neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu, kwa sababu giza linapita na ile nuru ya kweli tayari inang’aa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena nawaandikia amri mpya, neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu; kwa kuwa giza linapita na ile nuru ya kweli imekwisha kung'aa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata hivyo, amri hii ninayowaandikieni ni amri mpya, na ukweli wake unaonekana ndani ya Kristo na ndani yenu pia. Maana giza linatoweka, na mwanga wa kweli umekwisha anza kuangaza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena nawaandikia agizo jipya lililo kweli mwake namo mwenu ninyi, kwamba: Giza hupita, nao mwanga wa kweli umekwisha kumulika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena nawaandikia amri mpya, neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu; kwa kuwa giza linapita na ile nuru ya kweli imekwisha kung’aa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa ngambo ingine amri hii ninayowaandikia ni mupya, na ukweli wake unaonekana ndani ya Kristo na ndani yenu vilevile. Kwa maana giza linapita na mwangaza wa kweli umekwisha kutokea.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na ile amri ya zamani ndiyo ile mliyosikia tangu mwanzo. Tena nawaandikia amri mpya, neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu, kwa kuwa giza linapita na ile nuru ya kweli imekwisha kungʼaa.