1 John 3:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Oneni, basi, jinsi Baba alivyotupenda mno hata tunaitwa watoto wa Mungu! Na kweli, ndivyo tulivyo. Ndiyo maana ulimwengu haututambui sisi, kwani haumjui Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tazameni ni pendo kuu namna gani alilotupatia Baba, kwamba sisi tuitwe wana wa Mungu! Na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baba ametupenda sisi sana! Hili linaonesha jinsi anavyotupenda: Tunaitwa watoto wa Mungu. Ni kweli kuwa tu watoto wa Mungu. Lakini watu waliomo duniani hawaelewi ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu, kwa sababu hawamjui yeye.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Oneni basi, jinsi Baba alivyotupenda mno hata tunaitwa watoto wa Mungu! Na kweli, ndivyo tulivyo. Ndiyo maana ulimwengu haututambui sisi, kwani haumjui Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Oneni, basi, jinsi Baba alivyotupenda mno hata tunaitwa watoto wa Mungu! Na kweli, ndivyo tulivyo. Ndiyo maana ulimwengu haututambui sisi, kwani haumjui Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Oneni ni pendo kuu namna gani alilotupa Baba, kwamba sisi tuitwe watoto wa Mungu! Nasi ndivyo tulivyo. Sababu kwa nini ulimwengu haututambui, ni kwa kuwa haukumtambua yeye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tazameni ni pendo kuu namna gani alilotupa Baba, kwamba sisi tuitwe wana wa Mwenyezi Mungu! Na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Oneni, basi, jinsi Baba alivyotupenda mno hata tunaitwa watoto wa Mungu! Na kweli, ndivyo tulivyo. Ndiyo maana ulimwengu haututambui sisi, kwani haumjui Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Tazameni, jinsi Baba alivyotupenda sana, tuitwe watoto wa Mungu! Nasi ndio. Kwa hiyo ulimwengu haututambui, kwani haukumtambua yeye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muangalie namna Baba alivyoonyesha upendo wake kwetu hata tupate kuitwa watoto wa Mungu! Na kwa hakika sisi ndio wao! Ndiyo maana watu wa dunia hawatutambui, kwa sababu hawakumujua Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
FAHAMUNI, ni pendo la nanma gani alilotupa Baba, kuitwa wana wa Mungu. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.