1 John 3:15 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila anayemchukia ndugu yake ni muuaji; nanyi mnajua kwamba muuaji yeyote yule hana uhai wa milele ndani yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeyote amchukiaye ndugu yake ni muuaji, nanyi mwajua kwamba muuaji hana uzima wa milele ndani yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kila anayemchukia nduguye anayeamini ni muuaji. Nanyi mnajua kuwa hakuna muuaji aliye na uzima wa milele.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kila anayemchukia ndugu yake ni muuaji; nanyi mnajua kwamba muuaji yeyote yule hana uzima wa milele ndani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila anayemchukia ndugu yake ni muuaji; nanyi mnajua kwamba muuaji yeyote yule hana uhai wa milele ndani yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ye yote amchukiaye ndugu yake ni mwuaji, nanyi mwajua ya kwamba mwuaji hana uzima wa milele ndani yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeyote amchukiaye ndugu yake ni muuaji, nanyi mwajua ya kwamba muuaji hana uzima wa milele ndani yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukaao ndani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila anayemchukia ndugu yake ni muuaji; nanyi mnajua kwamba muuaji yeyote yule hana uhai wa milele ndani yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kila amchukiaye ndugu yake ni mwua watu, nanyi mwajua: hakuna mwua watu aliye mwenye uzima wa kale na kale, atakaoukalia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila mutu anayemuchukia ndugu yake ni mwuaji, nanyi munajua kwamba mwuaji yeyote hana uzima wa milele ndani yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Killa amchukiae ndugu yake ni mwuaji: nti mnajua ya kuwa mwuaji bana uzima wa milele ukikaa ndani yake.