1 John 3:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sisi tumepata kujua upendo ni nini, kwani Kristo aliyatoa maisha yake kwa ajili yetu. Nasi vilevile tunapaswa kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya ndugu zetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa namna hii twaweza kulijua pendo la Mungu: Kwa sababu Isa Al-Masihi aliutoa uhai wake kwa ajili yetu. Nasi imetupasa kuutoa uhai kwa ajili ya hao ndugu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivi ndivyo tunavyojua jinsi upendo wa kweli ulivyo: Yesu aliyatoa maisha yake kwa ajili yetu. Hivyo nasi tunapaswa kuyatoa maisha yetu, kwa ajili ya ndugu wa kike na wa kiume katika familia ya Kristo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sisi tumepata kujua upendo ni nini, kwani Kristo aliyatoa maisha yake kwa ajili yetu. Nasi vilevile tunapaswa kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya ndugu zetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sisi tumepata kujua upendo ni nini, kwani Kristo aliyatoa maisha yake kwa ajili yetu. Nasi vilevile tunapaswa kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya ndugu zetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa namna hii twaweza kulijua pendo la Mungu: Kwa sababu Yesu Kristo aliutoa uhai wake kwa ajili yetu. Nasi imetupasa kuutoa uhai kwa ajili ya hao ndugu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa namna hii twaweza kulijua pendo la Mwenyezi Mungu: Kwa sababu Isa Al-Masihi aliutoa uhai wake kwa ajili yetu. Nasi imetupasa kuutoa uhai kwa ajili ya hao ndugu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sisi tumepata kujua upendo ni nini, kwani Kristo aliyatoa maisha yake kwa ajili yetu. Nasi vilevile tunapaswa kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya ndugu zetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo ndipo, tulipoutambua upendo: Yeye aliitoa roho yake kwa ajili yetu; nasi imetupasa kuzitoa roho zetu kwa ajili ya ndugu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sisi tumetambua upendo kwa njia hii: Yesu Kristo alitoa uzima wake kwa ajili yetu. Nasi vilevile tunapaswa kutoa uzima wetu kwa ajili ya wandugu zetu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hivi tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliweka maisha yake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuweka maisha yetu kwa ajili ya ndugu.