1 John 3:24 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Anayezitii amri za Mungu anaishi katika muungano na Mungu na Mungu anaishi katika muungano naye. Kwa njia ya Roho ambaye Mungu ametujalia, sisi twajua kwamba Mungu anaishi katika muungano nasi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale wote wanaozishika amri zake hukaa ndani yake na yeye ndani yao. Hivi ndivyo tunavyojua kwamba anakaa ndani yetu. Nasi twajua hili kupitia kwa Roho wa Mungu, yule aliyetupatia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wote wanaozitii amri za Mungu wanaishi ndani ya Mungu. Na Mungu anaishi ndani yao. Tunajuaje kuwa Mungu anaishi ndani yetu? Tunajua kwa sababu ya Roho aliyetupa sisi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Anayezitii amri za Mungu anaishi katika muungano na Mungu na Mungu anaishi katika muungano naye. Kwa njia ya Roho ambaye Mungu ametujalia, sisi twajua kwamba Mungu anaishi katika muungano nasi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Anayezitii amri za Mungu anaishi katika muungano na Mungu na Mungu anaishi katika muungano naye. Kwa njia ya Roho ambaye Mungu ametujalia, sisi twajua kwamba Mungu anaishi katika muungano nasi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale wote wanaozishika amri zake hukaa ndani yake na yeye ndani yao. Hivi ndivyo tunavyojua kwamba anakaa ndani yetu. Nasi twajua hili kwa njia ya Roho yule aliyetupatia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale wote wanaozishika amri zake hukaa ndani yake na yeye ndani yao. Hivi ndivyo tunavyojua kwamba anakaa ndani yetu. Nasi twajua hili kwa njia ya Roho yule aliyetupa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Anayezitii amri za Mungu anaishi katika muungano na Mungu na Mungu anaishi katika muungano naye. Kwa njia ya Roho ambaye Mungu ametujalia, sisi twajua kwamba Mungu anaishi katika muungano nasi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye mwenye kuyashika maagizo yake hukaa mwake yeye, naye yeye mwake huyo. Hapo twatambua, ya kuwa yumo mwetu, tukiwa na Roho, aliyetupa sisi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu anayetii amri za Mungu anakaa ndani yake, na Mungu anakaa ndani ya yule mutu. Tunatambua kwamba Mungu anakaa ndani yetu kwa njia ya Roho Mutakatifu aliyetupatia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae azishikae amri zake hukaa ndani yake, nae ndani yake. Na hivi tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa Roho aliyotupa.