1 John 3:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, watoto wangu, msikubali kupotoshwa na mtu yeyote. Mtu atendaye matendo maadilifu ni mwadilifu kama vile Kristo alivyo mwadilifu kabisa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watoto wapendwa, mtu yeyote asiwadanganye. Kila mtu atendaye haki ana haki, kama yeye alivyo na haki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watoto wapendwa, msimruhusu mtu yeyote kuwadanganya. Kristo daima alitenda yaliyo haki. Hivyo kuwa mwema kama Kristo, ni lazima utende yaliyo haki.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, watoto wangu, msikubali kupotoshwa na mtu yeyote. Mtu atendaye matendo maadilifu ni mwadilifu kama vile Kristo alivyo mwadilifu kabisa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, watoto wangu, msikubali kupotoshwa na mtu yeyote. Mtu atendaye matendo maadilifu ni mwadilifu kama vile Kristo alivyo mwadilifu kabisa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watoto wadogo, mtu ye yote asiwadanganye. Kila mtu atendaye haki ana haki, kama yeye alivyo na haki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watoto wapendwa, mtu yeyote asiwadanganye. Kila mtu atendaye haki ana haki, kama yeye alivyo na haki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki ana haki, kama yeye alivyo na haki;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, watoto wangu, msikubali kupotoshwa na mtu yeyote. Mtu atendaye matendo maadilifu ni mwadilifu kama vile Kristo alivyo mwadilifu kabisa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vitoto, pasioneke mwenye kuwapoteza! Mwenye kufanya wongofu ni mwongofu, kama yeye alivyo mwongofu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watoto wangu, mutu asiwadanganye! Mutu anayetenda mambo ya haki ni mwenye haki kama vile Kristo ni mwenye haki.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wanangu, mtu asikudanganyeni; afanyae haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki;