1 John 3:9 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila aliye mtoto wa Mungu hatendi dhambi, maana anayo hali ya kimungu ndani yake; hawezi kutenda dhambi kwa sababu yeye ni mtoto wa Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeyote aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wa Mungu wakaa ndani yake, wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wale ambao ni watoto wa Mungu hawaendelei kutenda dhambi, kwa sababu wanayo maisha mapya waliyopewa na Mungu. Hawaendelei kutenda dhambi, kwa sababu wamefanyika watoto wa Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kila aliye mtoto wa Mungu hatendi dhambi, maana anayo hali ya kimungu ndani yake; hawezi kutenda dhambi kwa sababu yeye ni mtoto wa Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila aliye mtoto wa Mungu hatendi dhambi, maana anayo hali ya kimungu ndani yake; hawezi kutenda dhambi kwa sababu yeye ni mtoto wa Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ye yote aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wa Mungu wakaa ndani yake, wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeyote aliyezaliwa na Mwenyezi Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wa Mungu wakaa ndani yake, wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mwenyezi Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila aliye mtoto wa Mungu hatendi dhambi, maana anayo hali ya kimungu ndani yake; hawezi kutenda dhambi kwa sababu yeye ni mtoto wa Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kila aliyezaliwa naye Mungu hakosi, kwani mbegu zake hukaa mwake; kwa hiyo hawezi kukosa, maana alizaliwa naye Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila mutu anayekuwa mutoto wa Mungu hafanyi zambi, kwa sababu neno la Mungu linakaa ndani yake; tena hawezi kufanya zambi, maana Mungu ni baba yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Killa mtu aliyezaliwa na Mungu hafanyi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kufanya dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.