1 John 4:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hakuna mtu aliyekwisha mwona Mungu kamwe; lakini kama tukipendana, Mungu anaishi katika muungano nasi, na upendo wake unakamilika ndani yetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote. Lakini tukipendana, Mungu anakaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hakuna aliyemwona Mungu. Ila tukipendana sisi kwa sisi, Mungu anaishi ndani yetu. Kama tukipendana sisi kwa sisi, Upendo wa Mungu unafikia shabaha yake na unafanywa kamili ndani yetu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hakuna mtu aliyekwisha mwona Mungu kamwe; lakini kama tukipendana Mungu anaishi katika muungano nasi, na upendo wake unakamilika ndani yetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hakuna mtu aliyekwisha mwona Mungu kamwe; lakini kama tukipendana, Mungu anaishi katika muungano nasi, na upendo wake unakamilika ndani yetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hakuna mtu ye yote aliyemwona Mungu wakati wo wote. Kama tukipendana, Mungu anakaa ndani yetu na pendo lake limekamilika ndani yetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mwenyezi Mungu wakati wowote. Lakini tukipendana, Mungu anakaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hakuna mtu aliyekwisha mwona Mungu kamwe; lakini kama tukipendana, Mungu anaishi katika muungano nasi, na upendo wake unakamilika ndani yetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hakuna mtu aliyemwona Mungu hata kale; tukipendana, Mungu hukaa mwetu, upendo wake ukatimilika mwetu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hakuna hata mutu aliyekwisha kumwona Mungu wakati wowote. Tukipendana sisi kwa sisi, Mungu anaungana nasi na upendo wake unakamilika ndani yetu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo limekamilishwa ndani yetu.