1 John 4:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hii ndiyo njia ya kujua kama mtu anaongozwa na Roho wa Mungu: Kila anayekiri kwamba Kristo alikuja, akawa binadamu, mtu huyo anaye Roho wa Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivi ndivyo mnavyoweza kutambua Roho wa Mungu: Kila roho inayokubali kwamba Isa Al-Masihi amekuja katika mwili yatoka kwa Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivi ndivyo mwezavyo kuitambua Roho ya Mungu. Roho inayosema, “Naamini kuwa Yesu ni Masihi aliye kuja duniani na akafanyika mwanadamu.” Roho hiyo inatoka kwa Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hii ndiyo njia ya kujua kama mtu anaongozwa na Roho wa Mungu: Kila anayekiri kwamba Kristo alikuja, akawa binadamu, mtu huyo anaye Roho wa Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hii ndiyo njia ya kujua kama mtu anaongozwa na Roho wa Mungu: Kila anayekiri kwamba Kristo alikuja, akawa binadamu, mtu huyo anaye Roho wa Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivi ndivyo mnavyoweza kutambua Roho wa Mungu: Kila roho inayokubali kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatoka kwa Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivi ndivyo mnavyoweza kutambua Roho wa Mwenyezi Mungu: Kila roho inayokubali kwamba Isa Al-Masihi amekuja katika mwili yatoka kwa Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika hili mnamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hii ndiyo njia ya kujua kama mtu anaongozwa na Roho wa Mungu: Kila anayekiri kwamba Kristo alikuja, akawa binadamu, mtu huyo anaye Roho wa Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo ndipo, mtakapoitambua roho ya Mungu: kila roho inayoungama, ya kuwa Yesu Kristo amekuja mwenye mwili wa kimtu, imetoka kwa Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutatambua Roho wa Mungu kwa njia hii: kila mutu anayesadiki kwamba Yesu Kristo amekuja katika hali ya kimutu yuko na Roho wa Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hivi mwaijua Roho ya Mungu; killa roho iungamayo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu.