1 John 4:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini mtu yeyote asiyemkiri Kristo hivyo, hana huyo Roho atokaye kwa Mungu. Mtu huyo ana roho ambaye ni wa mpinzani wa Kristo; nanyi mlikwisha sikia kwamba anakuja, na sasa tayari amekwisha wasili ulimwenguni!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kila roho ambayo haimkubali Isa haitoki kwa Mungu. Hii ndiyo roho ya anayempinga Al-Masihi, ambayo mmesikia kwamba inakuja na sasa tayari iko ulimwenguni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Roho inayokataa kutamka hayo juu ya Yesu, hii ni roho iliyo adui kwa Kristo. Mmesikia kuwa adui wa kristo anakuja, na sasa amekwishakuja naye yupo tayari ulimwenguni.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini mtu yeyote asiyemkiri Kristo hivyo, hana huyo Roho atokaye kwa Mungu. Mtu huyo ana roho ambaye ni wa Adui wa Kristo; nanyi mlikwisha sikia kwamba anakuja, na sasa tayari amekwisha wasili ulimwenguni!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini mtu yeyote asiyemkiri Kristo hivyo, hana huyo Roho atokaye kwa Mungu. Mtu huyo ana roho ambaye ni wa mpinzani wa Kristo; nanyi mlikwisha sikia kwamba anakuja, na sasa tayari amekwisha wasili ulimwenguni!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kila roho ambayo haimkubali Yesu haitoki kwa Mungu. Hii ndiyo roho ya mpinga Kristo, ambayo mmesikia kwamba inakuja na sasa tayari iko ulimwenguni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kila roho ambayo haimkubali Isa haitoki kwa Mwenyezi Mungu. Hii ndiyo roho ya anayempinga Al-Masihi, ambayo mmesikia kwamba inakuja, na sasa tayari iko ulimwenguni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini mtu yeyote asiyemkiri Kristo hivyo, hana huyo Roho atokaye kwa Mungu. Mtu huyo ana roho ambaye ni wa mpinzani wa Kristo; nanyi mlikwisha sikia kwamba anakuja, na sasa tayari amekwisha wasili ulimwenguni!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kila roho isiyomwungama Yesu haikutoka kwa Mungu. Hiyo ndiyo roho ya Mpinga Kristo, mliyoisikia, ya kuwa inakuja; tena sasa imekwisha kuwamo humu ulimwenguni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mutu yeyote asiyemusadikia Yesu hana Roho anayetoka kwa Mungu. Mutu yule yuko na roho ya mupinga Kristo. Ninyi mumekwisha kusikia kwamba roho yule atakuja, na sasa amekwisha kuja katika dunia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na killa roho isiyoungama kwamba Yesu Kristo amekujii katika mwili, haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya adui wa Kristo ambae mmesikia kwamba yuaja; na sasa amekwisha kuwamo duniani.