1 John 4:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini sisi ni wake Mungu. Mtu anayemjua Mungu hutusikiliza, mtu asiye wa Mungu hatusikilizi. Basi, kwa njia hiyo tunaweza kutambua tofauti kati ya Roho wa ukweli na roho wa uongo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sisi twatokana na Mungu na yeyote anayemjua Mungu hutusikiliza, lakini asiyetokana na Mungu hatusikilizi. Hivi ndivyo tunavyoweza kutambua Roho wa Kweli na roho ya upotovu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sisi twatokana na Mungu. Yeye amjuaye Mungu atusikia; yeye asiyetokana na Mungu hatusikii. Katika hili twamjua Roho wa kweli, na roho ya upotevu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini sisi tunatokana na Mungu. Kwa hiyo watu wanaomjua Mungu hutusikia sisi. Lakini watu wasiotokana na Mungu hawatusikii sisi. Hivi ndivyo tunavyiojua Roho iliyo ya kweli na ile iliyo ya uongo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini sisi ni wake Mungu. Mtu anayemjua Mungu hutusikiliza, mtu asiye wa Mungu hatusikilizi. Basi, kwa njia hiyo tunaweza kutambua tofauti kati ya Roho wa ukweli na roho wa uongo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini sisi ni wake Mungu. Mtu anayemjua Mungu hutusikiliza, mtu asiye wa Mungu hatusikilizi. Basi, kwa njia hiyo tunaweza kutambua tofauti kati ya Roho wa ukweli na roho wa uongo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sisi twatokana na Mungu na ye yote anayemjua Mungu hutusikiliza, lakini asiyetokana na Mungu hatusikilizi. Hivi ndivyo tunavyoweza kutambua Roho wa Kweli na roho ya upotovu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sisi twatokana na Mwenyezi Mungu, na yeyote anayemjua Mungu hutusikiliza, lakini asiyetokana na Mwenyezi Mungu hatusikilizi. Hivi ndivyo tunavyoweza kutambua Roho wa Kweli na roho ya upotovu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sisi tunatokana na Mungu. Yeye amjuaye Mungu atusikia; yeye asiyetokana na Mungu hatusikii. Katika hili tunamjua Roho wa kweli, na roho ya upotevu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini sisi ni wake Mungu. Mtu anayemjua Mungu hutusikiliza, mtu asiye wa Mungu hatusikilizi. Basi, kwa njia hiyo tunaweza kutambua tofauti kati ya Roho wa ukweli na roho wa uongo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sisi tu wa Kimungu; naye amtambuaye Mungu hutusikia sisi, lakini asiye wa Kimungu hatusikii sisi. Hapo twaitambua roho, kama ni ya kweli au ya upotevu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sisi twatokana na Mungu. Yeye amjuaye Mungu atusikia; yeye asiyetokana na Mungu hatusikii. Katika hili twamjua Roho wa kweli, na roho ya upotevu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini sisi ni watu wa Mungu. Mutu anayemujua Mungu anatusikiliza; yule asiyemujua Mungu hatusikilizi. Basi ni kwa njia hii tunaweza kutambua tofauti kati ya Roho wa ukweli na roho ya udanganyifu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Sisi twatokana na Mungu. Yeye anijuae Mungu atusikia; yeye asiyetokana na Mungu hatusikii. Hivi twaijua Roho ya kweli, na roho ya upotevu.