1 John 4:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wapenzi wangu, tupendane, maana upendo hutoka kwa Mungu. Kila mtu aliye na upendo ni mtoto wa Mungu, na anamjua Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wapendwa, tupendane, kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu. Kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wapenzi rafiki, tunatakiwa tupendane sisi kwa sisi, kwa sababu upendo watoka kwa Mungu. Yeyote apendae amefanyika mwana wa Mungu. Na kila apendae anamfahamu Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wapenzi wangu, tupendane, maana upendo hutoka kwa Mungu. Kila mtu aliye na upendo ni mtoto wa Mungu, na anamjua Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wapenzi wangu, tupendane, maana upendo hutoka kwa Mungu. Kila mtu aliye na upendo ni mtoto wa Mungu, na anamjua Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wapenzi na tupendane, kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu. Kila apendaye amezaliwa na Mungu naye anamjua Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wapendwa, tupendane, kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu. Kila apendaye amezaliwa na Mwenyezi Mungu, naye anamjua Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wapenzi wangu, tupendane, maana upendo hutoka kwa Mungu. Kila mtu aliye na upendo ni mtoto wa Mungu, na anamjua Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wapendwa, tupendane sisi kwa sisi! Kwani upendo ni wa Kimungu. Kila mwenye kupenda amezaliwa naye Mungu, naye humtambua Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wapendwa wangu, tupendane, kwa maana upendo unatoka kwa Mungu. Kila mutu anayekuwa na upendo ni mutoto wa Mungu naye anamujua Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wapenzi, tupendane: kwa kuwa pendo ni la Mungu, na killa apendae amezaliwa na Mungu, nae anamjua Mungu.