1 John 4:9 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na Mungu alionesha upendo wake kwetu kwa kumtuma Mwanae wa pekee ulimwenguni, ili tuwe na uhai kwa njia yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivi ndivyo Mungu alivyoonesha pendo lake kwetu: Mungu alimtuma Mwanawe wa pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kupitia kwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivi ndivyo Mungu alivyo tuonyesha pendo lake sisi: Alimtuma mwanawe wa pekee ulimwenguni kutupatia sisi uzima katika yeye.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na Mungu alionyesha upendo wake kwetu kwa kumtuma Mwanae wa pekee ulimwenguni, ili tuwe na uzima kwa njia yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na Mungu alionesha upendo wake kwetu kwa kumtuma Mwanae wa pekee ulimwenguni, ili tuwe na uhai kwa njia yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivi ndivyo Mungu alivyoonyesha pendo lake kwetu, kwa sababu Mungu alimtuma Mwanawe wa pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivi ndivyo Mungu alivyoonyesha pendo lake kwetu: Mwenyezi Mungu alimtuma Mwanawe wa pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kupitia kwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na Mungu alionesha upendo wake kwetu kwa kumtuma Mwanae wa pekee ulimwenguni, ili tuwe na uhai kwa njia yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Upendo wake Mungu wa kutupenda sisi umeonekana waziwazi hapo, Mungu alipomtuma Mwana wake wa pekee kuja ulimwenguni, sisi tupewe naye uzima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hii ndiyo namna Mungu alivyoonyesha upendo wake kwetu: alimutuma Mwana wake wa pekee katika dunia kusudi kwa njia yake tupate uzima wa milele.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hivi pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwa kuwa Mungu amempeleka Mwana wake pekee ulimwenguni, tupate uzima kwa yeye.