1 John 5:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila mtu anayeamini kwamba Yesu ni Kristo, huyo ni mtoto wa Mungu. Kila anayempenda mzazi humpenda pia mtoto wa huyo mzazi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila mtu anayeamini kwamba Isa ndiye Al-Masihi amezaliwa na Mungu, na yeyote ampendaye Baba humpenda pia mtoto aliyezaliwa naye.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu wanao amini kuwa Yesu ni Masihi ni wana wa Mungu. Na kila ampendae Baba pia anawapenda watoto wa Baba.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kila mtu anayeamini kwamba Yesu ni Kristo, huyo ni mtoto wa Mungu; na, anayempenda mzazi humpenda pia mtoto wa huyo mzazi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila mtu anayeamini kwamba Yesu ni Kristo, huyo ni mtoto wa Mungu. Kila anayempenda mzazi humpenda pia mtoto wa huyo mzazi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila mtu anayeamini kwamba Yesu ndiye Kristo amezaliwa na Mungu na ye yote ampendaye Baba humpenda pia mtoto aliyezaliwa naye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila mtu anayeamini kwamba Isa ndiye Al-Masihi amezaliwa na Mungu, na yeyote ampendaye Baba humpenda pia mtoto aliyezaliwa naye.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila mtu anayeamini kwamba Yesu ni Kristo, huyo ni mtoto wa Mungu. Kila anayempenda mzazi humpenda pia mtoto wa huyo mzazi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Kila mwenye kuyategemea ya kwamba: Yesu ni Kristo, amezaliwa na Mungu. Naye kila mwenye kumpenda mzazi aliyemzaa humpenda hata yeye aliyezaliwa naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu yeyote anayeamini kwamba Yesu ndiye Kristo, yeye ni mutoto wa Mungu; na kila mutu anayemupenda baba anamupenda mwana wake vilevile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
KILLA mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na killa mtu ampendae mwenye kuzaa ampenda na yeye mwenye kuzaliwa nae.