1 John 5:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na sisi tuko thabiti mbele ya Mungu kwani tuna hakika kwamba tukimwomba chochote kadiri ya matakwa yake, yeye hutusikiliza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huu ndio ujasiri tulio nao tunapomkaribia Mungu, kwamba tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tunaweza kwenda kwa Mungu tukiwa na ujasiri huo. Hii ina maana kuwa tunapomwomba Mungu mambo (na mambo hayo yakakubaliana na matakwa yake kwetu), Mungu huyajali yale tunayosema.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na sisi tuko thabiti mbele ya Mungu kwani tuna hakika kwamba tukimwomba chochote kadiri ya mapenzi yake, yeye hutusikiliza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na sisi tuko thabiti mbele ya Mungu kwani tuna hakika kwamba tukimwomba chochote kadiri ya matakwa yake, yeye hutusikiliza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huu ndio ujasiri tulionao tunapomkaribia Mungu, kwamba kama tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huu ndio ujasiri tulio nao tunapomkaribia Mwenyezi Mungu, kwamba kama tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na sisi tuko thabiti mbele ya Mungu kwani tuna hakika kwamba tukimwomba chochote kadiri ya matakwa yake, yeye hutusikiliza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kunakotupa moyo wa kumjia wenye furaha ndiko kujua, yo yote, tutakayomwomba kwa hayo, ayatakayo, hutusikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nasi tuko na tumaini hili mbele ya Mungu: tunajua kwamba atatusikiliza tukimwomba kitu chochote kufuatana na mapenzi yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na huu ndio njasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu kama vile apendavyo, atusikia: