1 John 5:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeye hutusikiliza kila tunapomwomba; na kwa vile tunajua kwamba yeye hutusikiliza kila tunapomwomba, twajua pia kwamba hutupatia yote tunayomwomba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nasi kama tunajua atusikia, lolote tuombalo, tunajua kwamba tumekwisha kupata zile haja tulizomwomba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hutusikiliza kila wakati tunapomwomba. Hivyo tunatambua kuwa yeye hutupa kila tunachomwomba.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yeye hutusikiliza kila tunapomwomba; na kwa vile tunajua kwamba yeye hutusikiliza kila tunapomwomba, twajua pia kwamba atupatia yote tunayomwomba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeye hutusikiliza kila tunapomwomba; na kwa vile tunajua kwamba yeye hutusikiliza kila tunapomwomba, twajua pia kwamba hutupatia yote tunayomwomba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nasi kama tunajua ya kuwa atusikia, lo lote tuombalo, tunajua ya kwamba tumekwisha kupata zile haja tulizomwomba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nasi kama tunajua atusikia, lolote tuombalo, tunajua ya kwamba tumekwisha kupata zile haja tulizomwomba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kama tukijua kwamba atusikia, tunapoomba chochote, tunajua kwamba tumetimiziwa zile haja tulizomwomba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeye hutusikiliza kila tunapomwomba; na kwa vile tunajua kwamba yeye hutusikiliza kila tunapomwomba, twajua pia kwamba hutupatia yote tunayomwomba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nasi tukijua, ya kuwa anatusikia yo yote, tutakayomwomba, twajua: maombo, tuliyomwomba, tumekwisha kupewa.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, ikiwa tunajua kwamba anatusikiliza wakati tunapomwomba, tunajua vilevile kwamba anatupatia chochote tulichomwomba.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombapo cho chote, twajua kwamba tunazo zile dua tulizomwomba.