1 John 5:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
maana kila aliye mtoto wa Mungu anaweza kuushinda ulimwengu. Hivi ndivyo tunavyoushinda ulimwengu: Kwa imani yetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, yaani hiyo imani yetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
kwa sababu kila ambae ni mwana wa Mungu ana uwezo wa kushinda dhidi ya ulimwengu. Ni imani yetu iliyoshinda vita dhidi ya ulimwengu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
maana kila aliye mtoto wa Mungu anaweza kuushinda ulimwengu. Hivi ndivyo tunavyoushinda ulimwengu: kwa imani yetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
maana kila aliye mtoto wa Mungu anaweza kuushinda ulimwengu. Hivi ndivyo tunavyoushinda ulimwengu: kwa imani yetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, yaani, hiyo imani yetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana kila aliyezaliwa na Mwenyezi Mungu huushinda ulimwengu. Huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, yaani, hiyo imani yetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
maana kila aliye mtoto wa Mungu anaweza kuushinda ulimwengu. Hivi ndivyo tunavyoushinda ulimwengu: Kwa imani yetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Nako kunakotushindisha ulimwengu ndiko kumtegemea Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kwa sababu kila mutoto wa Mungu anashinda dunia. Tunashinda dunia kwa njia ya imani yetu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana killa kitu kilihozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, imani yetu.