1 Kings 1:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo, Nathani akamwendea Bathsheba mama yake Solomoni, akamwuliza, “Je, hujasikia kwamba Adoniya, mwanawe Hagithi, amejinyakulia mamlaka ya ufalme na bwana wetu Daudi hana habari?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Nathani akamuuliza Bathsheba, mama yake Sulemani, “Je, hujasikia kwamba Adoniya mwana wa Hagithi, amekuwa mfalme pasipo bwana wetu Daudi kujua jambo hili?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Nathani akamwambia Bath-sheba, mamaye Sulemani, akasema, Je! Hukusikia ya kuwa Adonia, mwana wa Hagithi, anamiliki, na bwana wetu Daudi hana habari?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo, Nathani akamwendea Bathsheba mama yake Solomoni, akamwuliza, “Je, hujasikia kwamba Adoniya, mwanawe Hagithi, amejinyakulia mamlaka ya ufalme na bwana wetu Daudi hana habari?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Nathani akamwuliza Bathsheba, mama yake Solomoni, “Je, hujasikia kwamba Adonia, mwana wa Hagathi, amekuwa mfalme pasipo bwana wetu Daudi kujua jambo hili?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Nathani akamuuliza Bathsheba, mama yake Sulemani, “Je, hujasikia kwamba Adoniya, mwana wa Hagithi, amekuwa mfalme pasipo bwana wetu Daudi kujua jambo hili?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Nathani akamwambia Bathsheba, mamaye Sulemani, akasema, Je! Hukusikia ya kuwa Adonia, mwana wa Hagithi, amekuwa mfalme, na bwana wetu Daudi hana habari?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo, Nathani akamwendea Bathsheba mama yake Solomoni, akamwuliza, “Je, hujasikia kwamba Adoniya, mwanawe Hagithi, amejinyakulia mamlaka ya ufalme na bwana wetu Daudi hana habari?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Natani alipomwambia Bati-Seba, mamake Salomo, kwamba: Hukusikia, ya kuwa Adonia, mwana wa Hagiti, amejipa ufalme, bwana wetu Dawidi asivijue?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Nathani akamwambia Bath-sheba, mamaye Sulemani, akasema, Je! Hukusikia ya kuwa Adonia, mwana wa Hagithi, anamiliki, na bwana wetu Daudi hana habari?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, Natani akamwendea Batiseba mama ya Solomono, akamwuliza: “Haujasikia kwamba Adonia mwana wa Hagiti amejiweka kuwa mufalme na bwana wetu Daudi hana habari?