1 Kings 1:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwendee mfalme Daudi, umwulize, ‘Je, bwana wangu mfalme, hukuniapia mimi mtumishi wako ukisema, “Mwana wako Solomoni atatawala mahali pangu na atakaa juu ya kiti changu cha enzi?” Imekuwaje basi, sasa Adoniya anatawala?’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ingia kwa Mfalme Daudi na umwambie, ‘Bwana wangu mfalme, je hukuniapia mimi mtumishi wako: “Hakika mwanao Sulemani atakuwa mfalme baada yangu na ndiye atakayeketi kwenye kiti changu cha ufalme”? Kwa nini basi Adoniya amekuwa mfalme?’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Enenda uingie ndani kwa mfalme Daudi, ukamwambie, Je! Hukuniapia mimi mjakazi wako, Ee mfalme, bwana wangu, kusema, Hakika yake Sulemani mwana wako atamiliki baada yangu, na kuketi katika kiti changu cha enzi? Mbona basi anamiliki Adonia?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwendee mfalme Daudi, umwulize, ‘Je, bwana wangu mfalme, hukuniapia mimi mtumishi wako ukisema, “Mwana wako Solomoni atatawala mahali pangu na atakaa juu ya kiti changu cha enzi?” Imekuwaje basi, sasa Adoniya anatawala?’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ingia kwa Mfalme Daudi na umwambie, ‘Bwana wangu mfalme, je hukuniapia mimi mtumishi wako: “Hakika mwanao Solomoni atakuwa mfalme baada yangu na ndiye atakayeketi juu ya kiti changu cha ufalme”? Kwa nini basi Adonia amekuwa mfalme?’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ingia kwa Mfalme Daudi na umwambie, ‘Bwana wangu mfalme, je hukuniapia mimi mtumishi wako: “Hakika mwanao Sulemani atakuwa mfalme baada yangu na ndiye atakayeketi juu ya kiti changu cha ufalme”? Kwa nini basi Adoniya amekuwa mfalme?’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nenda uingie ndani kwa mfalme Daudi, ukamwambie, Je! Hukuniapia mimi mjakazi wako, Ee mfalme, bwana wangu, kusema, Hakika yake Sulemani mwana wako atamiliki baada yangu, na kuketi katika kiti changu cha enzi? Mbona basi anamiliki Adonia?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwendee mfalme Daudi, umwulize, ‘Je, bwana wangu mfalme, hukuniapia mimi mtumishi wako ukisema, “Mwana wako Solomoni atatawala mahali pangu na atakaa juu ya kiti changu cha enzi?” Imekuwaje basi, sasa Adoniya anatawala?’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nenda, uingie mwake mfalme Dawidi, umwambie: Je? Wewe, bwana wangu mfalme, hukumwapia kijakazi wako kwamba: Mwanao Salomo atakuwa mfalme nyuma yangu, yeye akae katika kiti changu cha kifalme? Mbona Adonia amekwisha kujipa ufalme?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Enenda uingie ndani kwa mfalme Daudi, ukamwambie, Je! Hukuniapia mimi mjakazi wako, Ee mfalme, bwana wangu, kusema, Hakika yake Sulemani mwana wako atamiliki baada yangu, na kuketi katika kiti changu cha enzi? Mbona basi anamiliki Adonia?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Umwendee mufalme Daudi, umwulize: ‘Bwana wangu mufalme, si uliniapia mimi mujakazi wako ukisema: Mwana wako Solomono atatawala nyuma yangu, na ataikaa juu ya kiti changu cha kifalme? Imekuwa namna gani basi, sasa Adonia anatawala?’