1 Kings 1:30 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kama nilivyokuapia mbele za Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nikisema, ‘Mwanao Solomoni atatawala baada yangu, na kwamba atakaa juu ya kiti changu cha enzi badala yangu,’ ndivyo nitakavyofanya leo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
hakika nitatekeleza leo kile nilichokuapia kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: Mwanao Sulemani atakuwa mfalme baada yangu, naye ataketi kwenye kiti changu cha ufalme baada yangu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
hakika yake nitafanya leo kama vile nilivyokuapia kwa Bwana, Mungu wa Israeli, nikasema, Kwa yakini Sulemani mwanao atamiliki baada yangu, naye ndiye atakayeketi katika kiti changu cha enzi badala yangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kama nilivyokuapia mbele za Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nikisema, ‘Mwanao Solomoni atatawala baada yangu, na kwamba atakaa juu ya kiti changu cha enzi badala yangu,’ ndivyo nitakavyofanya leo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
hakika nitatekeleza leo kile nilichokuapia kwa BWANA, Mungu wa Israeli: Mwanao Solomoni atakuwa mfalme baada yangu, naye ataketi kwenye kiti changu cha ufalme baada yangu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
hakika nitatekeleza leo kile nilichokuapia kwa bwana, Mungu wa Israeli: Mwanao Sulemani atakuwa mfalme baada yangu, naye ataketi kwenye kiti changu cha ufalme baada yangu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
hakika yake nitafanya leo kama vile nilivyokuapia kwa BWANA, Mungu wa Israeli, nikasema, Kwa hakika Sulemani mwanao atamiliki baada yangu, naye ndiye atakayeketi katika kiti changu cha enzi badala yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
kama nilivyokuapia mbele za Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nikisema, ‘Mwanao Solomoni atatawala baada yangu, na kwamba atakaa juu ya kiti changu cha enzi badala yangu,’ ndivyo nitakavyofanya leo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
siku hii ya leo nitavifanya, nilivyokuapia na kumtaja Bwana Mungu wa Isiraeli kwamba: Mwanao Salomo atakuwa mfalme nyuma yangu, yeye akae katika kiti changu cha kifalme mahali pangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
hakika yake nitafanya leo kama vile nilivyokuapia kwa BWANA, Mungu wa Israeli, nikasema, Kwa yakini Sulemani mwanao atamiliki baada yangu, naye ndiye atakayeketi katika kiti changu cha enzi badala yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kama nilivyokuapia mbele ya Yawe, Mungu wa Israeli, nikisema: ‘Mwana wako Solomono atatawala nyuma yangu, na ataikaa juu ya kiti changu cha kifalme pahali pangu’, ndivyo nitakavyofanya leo.”