1 Kings 1:34 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
halafu umruhusu kuhani Sadoki na nabii Nathani wampake mafuta kuwa mfalme wa Israeli; baadaye pigeni tarumbeta na kusema, ‘Mfalme Solomoni aishi!’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huko kuhani Sadoki na nabii Nathani wampake mafuta awe mfalme juu ya Israeli. Pigeni tarumbeta na mpaze sauti, mkisema, ‘Mfalme Sulemani aishi maisha marefu!’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kisha Sadoki, kuhani, na Nathani, nabii, na wamtie mafuta huko, awe mfalme juu ya Israeli; kapigeni panda, mkaseme, Mfalme Sulemani na aishi!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
halafu umruhusu kuhani Sadoki na nabii Nathani wampake mafuta kuwa mfalme wa Israeli; baadaye pigeni tarumbeta na kusema, ‘Mfalme Solomoni aishi!’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huko kuhani Sadoki na nabii Nathani wamtie mafuta awe mfalme juu ya Israeli. Pigeni tarumbeta na mpaze sauti, ‘Mfalme Solomoni aishi maisha marefu!’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huko kuhani Sadoki na nabii Nathani wamtie mafuta awe mfalme juu ya Israeli. Pigeni tarumbeta na mpaze sauti, ‘Mfalme Sulemani aishi maisha marefu!’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kisha Sadoki, kuhani, na Nathani, nabii, na wamtie mafuta huko, awe mfalme juu ya Israeli; kapigeni panda, mkaseme, Mfalme Sulemani na aishi!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
halafu umruhusu kuhani Sadoki na nabii Nathani wampake mafuta kuwa mfalme wa Israeli; baadaye pigeni tarumbeta na kusema, ‘Mfalme Solomoni aishi!’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huko mtambikaji Sadoki na mfumbuaji Natani wampake mafuta, awe mfalme wa Waisiraeli. Kisha mtapiga mabaragumu kwamba: Pongezi, mfalme Salomo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kisha Sadoki, kuhani, na Nathani, nabii, na wamtie mafuta huko, awe mfalme juu ya Israeli; kapigeni panda, mkaseme, Mfalme Sulemani na aishi!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu umuruhusu kuhani Zadoki na nabii Natani wamupakae mafuta akuwe mufalme wa Israeli. Kisha mupige baragumu na kusema: ‘Mufalme Solomono aishi!’