1 Kings 1:45 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kisha kuhani Sadoki na nabii Nathani wamemtia mafuta kuwa mfalme kule Gihoni; halafu wametoka hapo wakifurahi; ndicho kisa cha makelele hayo unayosikia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
nao kuhani Sadoki na nabii Nathani wamempaka mafuta huko Gihoni kuwa mfalme. Kutoka hapo wamepanda wakishangilia, na sauti zimeenea kote katika mji. Hizo ndizo kelele unazosikia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Sadoki, kuhani, na Nathani, nabii, wakamtia mafuta huko Gihoni, ili awe mfalme. Nao wamepanda juu kutoka huko wakifurahi, hata mji ukavuma. Ndizo kelele zile mlizozisikia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kisha kuhani Sadoki na nabii Nathani wamemtia mafuta kuwa mfalme kule Gihoni; halafu wametoka hapo wakifurahi; ndicho kisa cha makelele hayo unayosikia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
nao kuhani Sadoki na nabii Nathani wamemtia mafuta kuwa mfalme huko Gihoni. Kuanzia hapo wameendelea kushangilia na sauti zimeenea pote mjini. Hizo ndizo kelele unazosikia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
nao kuhani Sadoki na nabii Nathani wamemtia mafuta kuwa mfalme huko Gihoni. Kuanzia hapo wameendelea kushangilia na sauti zimeenea pote mjini. Hizo ndizo kelele unazosikia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Sadoki, kuhani, na Nathani, nabii, wakamtia mafuta huko Gihoni, ili awe mfalme. Nao wamepanda juu kutoka huko wakifurahi, hata mji ukavuma. Ndizo kelele zile mlizozisikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
kisha kuhani Sadoki na nabii Nathani wamemtia mafuta kuwa mfalme kule Gihoni; halafu wametoka hapo wakifurahi; ndicho kisa cha makelele hayo unayosikia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtambikaji Sadoki na mfumbuaji Natani wakampaka mafuta kule Gihoni, awe mfalme, kisha wakapanda kutoka huko wenye furaha, mji ukavuma; hizo ndizo sauti, mlizozisikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Sadoki, kuhani, na Nathani, nabii, wakamtia mafuta huko Gihoni, ili awe mfalme. Nao wamepanda juu kutoka huko wakifurahi, hata mji ukavuma. Ndizo kelele zile mlizozisikia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha kuhani Zadoki na nabii Natani wakamupakaa mafuta akuwe mufalme kule Gihoni. Halafu wametoka hapo wakifurahi, ndiyo sababu ya makelele hayo unayosikia.