1 Kings 1:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo, Adoniya, mwana wa Daudi na Hagithi, akaanza kujigamba kwamba yeye ndiye atakayekuwa mfalme. Basi, akajitayarishia magari ya kukokotwa, wapandafarasi na wapiga mbio hamsini wa kumtangulia na kumshangilia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Adoniya mwana wa Hagithi akajigamba na kusema, “Mimi nitakuwa mfalme.” Hivyo akaweka tayari magari ya vita na wapanda farasi, pamoja na watu hamsini wa kumtangulia wakikimbia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Adonia mwana wa Hagithi akatakabari, akasema, Mimi nitakuwa mfalme. Akajiwekea tayari magari na wapanda farasi, na watu hamsini wapige mbio mbele yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo, Adoniya, mwana wa Daudi na Hagithi, akaanza kujigamba kwamba yeye ndiye atakayekuwa mfalme. Basi, akajitayarishia magari ya kukokotwa, wapandafarasi na wapiga mbio hamsini wa kumtangulia na kumshangilia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Adonia, ambaye mama yake alikuwa Hagathi, akajigamba na kusema, “Mimi nitakuwa mfalme.” Hivyo akajiwekea tayari magari na wapanda farasi, pamoja na watu hamsini watakaomtangulia wakikimbia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Adoniya, ambaye mama yake alikuwa Hagithi, akajigamba na kusema, “Mimi nitakuwa mfalme.” Hivyo akajiwekea tayari magari na wapanda farasi, pamoja na watu hamsini wa kumtangulia wakikimbia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Adonia mwana wa Hagithi akatakabari, akasema, Mimi nitakuwa mfalme. Akajiwekea tayari magari na wapanda farasi, na watu hamsini wapige mbio mbele yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo, Adoniya, mwana wa Daudi na Hagithi, akaanza kujigamba kwamba yeye ndiye atakayekuwa mfalme. Basi, akajitayarishia magari ya kukokotwa, wapandafarasi na wapiga mbio hamsini wa kumtangulia na kumshangilia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Adonia, mwana wa Hagiti, akajikweza kwamba: Mimi nitakuwa mfalme, akajipatia magari na farasi na watu 50, wamtangulie kwa kupiga mbio.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Adonia mwana wa Hagithi akatakabari, akasema, Mimi nitakuwa mfalme. Akajiwekea tayari magari na wapanda farasi, na watu hamsini wapige mbio mbele yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati ule, Adonia mwana wa Daudi kutoka muke wake Hagiti, akaanza kujivuna kwamba yeye ndiye atakayekuwa mufalme. Basi, akajitayarishia magari, wapanda-farasi na watu makumi tano wa kumutangulia.