1 Kings 1:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku moja, Adoniya alitoa sadaka ya kondoo, ng'ombe na ndama wanono kwenye Jiwe la Nyoka, karibu na chemchemi iitwayo Enrogeli. Akawaalika kwenye karamu ya sadaka hiyo ndugu zake wote, yaani wana wengine wa mfalme, na watumishi wote wa mfalme waliokuwa wa kabila la Yuda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Adoniya akatoa dhabihu ya kondoo, ng’ombe na ndama walionona kwenye Jiwe la Zohelethi karibu na En-Rogeli. Akawaalika ndugu zake wote wana wa mfalme, na wanaume wote wa Yuda waliokuwa maafisa wa mfalme,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Adonia akachinja kondoo, na ng'ombe, na vinono, karibu na jiwe la Zohelethi, lililo karibu na chemchemi Rogeli; akawaita ndugu zake wote, wana wa mfalme, na watu wote wa Yuda, watumishi wa mfalme;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku moja, Adoniya alitoa sadaka ya kondoo, ng'ombe na ndama wanono kwenye Jiwe la Nyoka, karibu na chemchemi iitwayo Enrogeli. Akawaalika kwenye karamu ya sadaka hiyo ndugu zake wote, yaani wana wengine wa mfalme, na watumishi wote wa mfalme waliokuwa wa kabila la Yuda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Adonia akatoa dhabihu ya kondoo, ng'ombe na ndama walionona kwenye Jiwe la Zohelethi karibu na En-Rogeli. Akawaalika ndugu zake wote, wana wa mfalme na wanaume wote wa Yuda waliokuwa maafisa wa kifalme,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Adoniya akatoa dhabihu ya kondoo, ng’ombe na ndama walionona kwenye Jiwe la Zohelethi karibu na En-Rogeli. Akawaalika ndugu zake wote, wana wa mfalme na wanaume wote wa Yuda waliokuwa maafisa wa mfalme,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Adonia akatoa sadaka ya kondoo, ng'ombe na ndama wanono, karibu na jiwe la Zohelethi, lililo karibu na chemchemi Enrogeli; akawaita ndugu zake wote, wana wa mfalme, na watu wote wa Yuda, watumishi wa mfalme;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku moja, Adoniya alitoa sadaka ya kondoo, ng'ombe na ndama wanono kwenye Jiwe la Nyoka, karibu na chemchemi iitwayo Enrogeli. Akawaalika kwenye karamu ya sadaka hiyo ndugu zake wote, yaani wana wengine wa mfalme, na watumishi wote wa mfalme waliokuwa wa kabila la Yuda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Adonia akatambika penye Jiwe la Zoheleti (Mwamba wa Nyoka) karibu na Eni-Rogeli (Chemchemi ya Wafua nguo) na kuchinja kondoo na ng'ombe na vinono, akawaalika ndugu zake wote waliokuwa wana wa mfalme wa waume wote wa Yuda waliomtumikia mfalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Adonia akachinja kondoo, na ng’ombe, na vinono, karibu na jiwe la Zohelethi, lililo karibu na chemchemi Rogeli; akawaita ndugu zake wote, wana wa mfalme, na watu wote wa Yuda, watumishi wa mfalme;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku moja, Adonia alitoa sadaka ya kondoo, ngombe na wana-ngombe wanono kwenye Jiwe la Zoheleti, karibu na chemichemi inayoitwa Enrogeli. Akawaalika kwenye karamu ya sadaka hiyo wandugu zake wote, ni kusema wana wengine wa mufalme, na watumishi wote wa mufalme wanaokuwa wa kabila la Yuda.