1 Kings 10:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye mfalme aliitumia miti hiyo ya msandali kwa ajili ya nguzo za nyumba ya Mwenyezi-Mungu, na za ikulu na pia kwa kutengenezea vinubi na vinanda vya waimbaji. Kiasi cha miti ya msandali kama hicho hakijaonekana tena mpaka leo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme alitumia miti ya msandali kutengenezea nguzo za Hekalu la Mwenyezi Mungu na za jumba la kifalme, na kutengenezea vinubi na zeze kwa ajili ya waimbaji. Miti mingi ya msandali kiasi hicho haijawahi kuletwa au kuonekana tangu wakati ule.)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme akafanya kwa mia hiyo ya msandali nguzo za nyumba ya Bwana, na za nyumba ya mfalme, na vinubi na vinanda vya hao waimbaji; wala haikuja miti ya msandali kama hiyo, wala haikuonekana, hata leo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye mfalme aliitumia miti hiyo ya msandali kwa ajili ya nguzo za nyumba ya Mwenyezi-Mungu, na za ikulu na pia kwa kutengenezea vinubi na vinanda vya waimbaji. Kiasi cha miti ya msandali kama hicho hakijaonekana tena mpaka leo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akatumia miti ya msandali kuwa nguzo kwa ajili ya Hekalu la BWANA na kwa jumba la kifalme, pia kwa kutengeneza vinubi na zeze kwa ajili ya waimbaji. Kiasi hicho kingi cha miti ya msandali hakijawahi kuingizwa nchini tangu siku ile.)
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akatumia miti ya msandali kuwa nguzo ya Hekalu la bwana na kwa jumba la kifalme, pia kwa kutengeneza vinubi na zeze kwa ajili ya waimbaji. Kiasi hicho kingi cha msandali hakijawahi kuingizwa au kuonekana humo tangu siku ile.)
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mfalme akafanya kwa miti hiyo ya msandali nguzo za nyumba ya BWANA, na za nyumba ya mfalme, na vinubi na vinanda vya hao waimbaji; wala haikuja miti ya msandali kama hiyo, wala haikuonekana, hata leo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye mfalme aliitumia miti hiyo ya msandali kwa ajili ya nguzo za nyumba ya Mwenyezi-Mungu, na za ikulu na pia kwa kutengenezea vinubi na vinanda vya waimbaji. Kiasi cha miti ya msandali kama hicho hakijaonekana tena mpaka leo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye mfalme akaitumia hiyo miti ya uvumba ya kuzikingia baraza za Nyumba ya Bwana na za nyumba ya mfalme na ya kutengeneza mazeze na mapango ya waimbaji. Miti ya uvumba kama hiyo ilikuwa haijaingia huko bado, wala haikuonekana tena hata siku hii ya leo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme akafanya kwa mia hiyo ya msandali nguzo za nyumba ya BWANA, na za nyumba ya mfalme, na vinubi na vinanda vya hao waimbaji; wala haikuja miti ya msandali kama hiyo, wala haikuonekana, hata leo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye mufalme aliitumia miti hiyo ya musandali kwa ajili ya nguzo za nyumba ya Yawe, na za nyumba ya kifalme na vilevile kwa kutengeneza vinubi na vinanda vya waimbaji. Kiasi cha miti ya musandali kama hicho hakijaonekana tena mpaka leo.