1 Kings 10:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aliwasili akiwa amefuatana na msafara wa watu pamoja na ngamia waliobeba manukato, zawadi nyingi sana na vito vya thamani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alifika Yerusalemu akiwa na msafara mkubwa sana wenye ngamia waliobeba vikolezo, dhahabu nyingi, na vito vya thamani. Akaenda kwa Sulemani na kuzungumza naye mambo yote aliyokuwa nayo moyoni mwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaingia Yerusalemu na wafuasi wengi sana, na ngamia wachukuao manukato, na dhahabu nyingi sana, na vito vya thamani; alipomfikilia Sulemani, akazungumza naye mambo yote aliyokuwa nayo moyoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aliwasili akiwa amefuatana na msafara wa watu pamoja na ngamia waliobeba manukato, zawadi nyingi sana na vito vya thamani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipofika Yerusalemu pamoja na msafara mkubwa sana: pamoja na ngamia waliobeba vikolezi, kiasi kikubwa cha dhahabu na vito vya thamani; alikuja kwa Solomoni na kuzungumza naye kuhusu yote ambayo alikuwa nayo moyoni mwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alifika Yerusalemu akiwa na msafara mkubwa sana: pamoja na ngamia waliobeba vikolezi, kiasi kikubwa cha dhahabu na vito vya thamani; alikuja kwa Sulemani na kuzungumza naye kuhusu yote ambayo alikuwa nayo moyoni mwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaingia Yerusalemu na wafuasi wengi sana, na ngamia wachukuao manukato, na dhahabu nyingi sana, na vito vya thamani; alipomfikia Sulemani, akazungumza naye mambo yote aliyokuwa nayo moyoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aliwasili akiwa amefuatana na msafara wa watu pamoja na ngamia waliobeba manukato, zawadi nyingi sana na vito vya thamani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaja Yerusalemu na vikosi vikubwa mno na ngamia waliochukua uvumba na dhahabu nyingi sana na vito. Alipofika kwa Salomo akasema naye na kumwuliza yote, aliyokuwa nayo moyoni mwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaingia Yerusalemu na wafuasi wengi sana, na ngamia wachukuao manukato, na dhahabu nyingi sana, na vito vya thamani; alipomfikilia Sulemani, akazungumza naye mambo yote aliyokuwa nayo moyoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akafika Yerusalema akisindikizwa na watu wengi sana pamoja na ngamia waliobeba marasi, zawadi nyingi sana, zahabu na mawe ya bei kali.