1 Kings 10:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kulikuwa pia na sanamu kumi na mbili za simba zimesimama, moja mwishoni mwa kila ngazi. Kiti kama hicho hakijawahi kutengenezwa katika ufalme wowote ule.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Simba kumi na wawili walisimama kwenye ngazi sita, mmoja katika kila upande wa kila ngazi. Hakuna kiti kama hicho kiliwahi kutengenezwa katika ufalme mwingine wowote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na simba kumi na wawili wamesimama juu ya daraja sita huko na huko; wala hakikufanyika kwa mkono wake katika ufalme wo wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kulikuwa pia na sanamu kumi na mbili za simba zimesimama, moja mwishoni mwa kila ngazi. Kiti kama hicho hakijawahi kutengenezwa katika ufalme wowote ule.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Simba kumi na wawili walisimama kwenye ngazi sita, wawili kwenye kila ngazi, yaani, mmoja upande huu na mwingine upande huu. Hakuna kitu kama hicho kilichokuwa kimefanyika kwenye ufalme mwingine wo wote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Simba kumi na wawili walisimama kwenye ngazi sita, mmoja katika kila upande wa kila ngazi. Hakuna kitu kama hicho kilichokuwa kimefanyika kwenye ufalme mwingine wowote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na simba kumi na wawili wamesimama juu ya ngazi sita huku na huko; wala hakikufanyika kwa mkono wake katika ufalme wowote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kulikuwa pia na sanamu kumi na mbili za simba zimesimama, moja mwishoni mwa kila ngazi. Kiti kama hicho hakijawahi kutengenezwa katika ufalme wowote ule.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena mifano kumi na miwili ya simba ilikuwa imesimama juu ya vile vipago sita, huku na huko. Kitu kilichotengenezwa vizuri hivyo hakikuwako katika ufalme wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na simba kumi na wawili wamesimama juu ya daraja sita huko na huko; wala hakikufanyika kwa mkono wake katika ufalme wo wote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulikuwa vilevile sanamu kumi na mbili za simba wamesimama, mumoja kwa mwisho wa kila ngazi. Kiti kama hicho kilikuwa bado hakijatengenezwa katika ufalme wowote.