1 Kings 10:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Solomoni alikusanya magari ya farasi na wapandafarasi, alikuwa na magari ya farasi 1,400 na wapandafarasi 12,000 ambao aliwaweka katika miji yenye vituo vya magari ya farasi, na huko Yerusalemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sulemani alikusanya magari ya vita na farasi. Akawa na magari ya vita elfu moja mia nne, na farasi elfu kumi na mbili, ambayo aliyaweka katika miji ya magari ya vita, na mengine akawa nayo huko Yerusalemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sulemani akakusanya magari na wapandao farasi; naye alikuwa na magari elfu na mia nne, na wapandao farasi kumi na mbili elfu, aliowaweka katika miji ya magari, na pamoja na mfalme huko Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Solomoni alikusanya magari ya farasi na wapandafarasi, alikuwa na magari ya farasi 1,400 na wapandafarasi 12,000 ambao aliwaweka katika miji yenye vituo vya magari ya farasi, na huko Yerusalemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Solomoni akalimbikiza magari makubwa mazuri na farasi; alikuwa na magari 1,400 na farasi 12,000 ambayo aliyaweka katika miji ya magari pia pamoja naye huko Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sulemani akakusanya magari ya vita na farasi. Alikuwa na magari 1,400 na farasi 12,000, ambayo aliyaweka katika miji ya magari na mengine akawa nayo huko Yerusalemu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sulemani akakusanya magari na wapandao farasi; naye alikuwa na magari elfu moja mia nne, na wapandao farasi elfu kumi na mbili, aliowaweka katika miji ya magari, na pamoja na mfalme huko Yerusalemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Solomoni alikusanya magari ya farasi na wapandafarasi, alikuwa na magari ya farasi 1,400 na wapandafarasi 12,000 ambao aliwaweka katika miji yenye vituo vya magari ya farasi, na huko Yerusalemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Salomo akakusanya magari na wapanda farasi, hata akawa na magari 1400 na wapanda farasi 12000, akawakalisha katika miji ya magari namo mwake mfalme mle Yerusalemu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sulemani akakusanya magari na wapandao farasi; naye alikuwa na magari elfu na mia nne, na wapandao farasi kumi na mbili elfu, aliowaweka katika miji ya magari, na pamoja na mfalme huko Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Solomono alikusanya magari ya vita na waaskari wapanda-farasi. Alikuwa na magari ya vita elfu moja na mia ine na waaskari wapanda-farasi elfu kumi na mbili ambao aliwaweka katika miji yenye vituo vya magari ya vita, na kule Yerusalema.