1 Kings 10:29 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Gari moja la kukokotwa liliweza kununuliwa huko Misri kwa fedha ipatayo kilo 7, na farasi mmoja aliweza kugharimu fedha kilo 2. Wafanyabiashara wa mfalme walisafirisha magari na farasi hao na kuwauzia wafalme wote wa Wahiti na wa Wasiria.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walinunua magari ya vita kutoka Misri kwa shekeli mia sita za fedha kila moja, na kila farasi kwa shekeli mia moja na hamsini; na wakawauzia wafalme wote wa Wahiti na wa Waaramu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena gari huja kutoka katika Misri kwa shekeli mia sita za fedha, na farasi mmoja kwa mia hamsini; vivyo watu wakawaletea wafalme wote wa Wahiti, na wafalme wa Shamu, mikononi mwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Gari moja la kukokotwa liliweza kununuliwa huko Misri kwa fedha ipatayo kilo 7, na farasi mmoja aliweza kugharimu fedha kilo 2. Wafanyabiashara wa mfalme walisafirisha magari na farasi hao na kuwauzia wafalme wote wa Wahiti na wa Wasiria.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waliingiza magari kutoka Misri kwa bei ya shekeli za fedha 600 na farasi kwa shekeli za fedha 150. Pia waliwauza nje kwa wafalme wote wa Wahiti na Waaramu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waliagiza magari kutoka Misri kwa bei ya shekeli 600 za fedha na farasi kwa shekeli 150. Pia waliwauza nje kwa wafalme wote wa Wahiti na wa Waaramu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena gari huja kutoka Misri kwa shekeli mia sita za fedha, na farasi mmoja kwa mia moja na hamsini; hivyo basi watu wakawaletea wafalme wote wa Wahiti, na wafalme wa Shamu, mikononi mwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Gari moja la kukokotwa liliweza kununuliwa huko Misri kwa fedha ipatayo kilo 7, na farasi mmoja aliweza kugharimu fedha kilo 2. Wafanyabiashara wa mfalme walisafirisha magari na farasi hao na kuwauzia wafalme wote wa Wahiti na wa Wasiria.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Magari yaliyokuja kutoka Misri moja lilikuwa fedha 600 na farasi mmoja fedha 150. Vivyo hivyo waliwapelekea nao wafalme wote wa Wahiti na wafalme wa Ushami kwa mikono yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena gari huja kutoka katika Misri kwa shekeli mia sita za fedha, na farasi mmoja kwa mia hamsini; vivyo watu wakawaletea wafalme wote wa Wahiti, na wafalme wa Shamu, mikononi mwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Gari moja liliweza kununuliwa kule Misri kwa feza inayopita kilo saba, na farasi mumoja aliweza kununuliwa kwa feza kilo mbili. Wachuuzi wa mufalme walisafirisha magari na farasi hao na kuwauzishia wafalme wote wa Wahiti na wa Waaramu.