1 Kings 10:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Solomoni akayajibu maswali yote; hapakuwa na swali lolote lililomshinda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sulemani alimjibu maswali yake yote; hapakuwa na jambo lolote lililokuwa gumu kwa mfalme hata asiweze kumwelezea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Sulemani akamfumbulia maswali yake yote; wala hakukuwa na neno alilofichiwa mfalme asimwambie.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Solomoni akayajibu maswali yote; hapakuwa na swali lolote lililomshinda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Solomoni akamjibu maswali yake yote, hakukuwa na jambo lo lote lililokuwa gumu kwa mfalme asiweze kumwelezea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sulemani akamjibu maswali yake yote, hakukuwa na jambo lolote lililokuwa gumu kwa mfalme asiweze kumwelezea.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Sulemani akamfumbulia maswali yake yote; wala hakukuwa na neno aliloshindwa mfalme asimwambie.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Solomoni akayajibu maswali yote; hapakuwa na swali lolote lililomshinda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Salomo akamwelezea yote, aliyomwuliza, halikuwako neno lililofichika maana kwake mfalme, asiloweza kumwelezea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Sulemani akamfumbulia maswali yake yote; wala hakukuwa na neno alilofichiwa mfalme asimwambie.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Solomono akayajibu maulizo yote; hakuna hata ulizo moja lililomushinda.