1 Kings 10:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
tena alipoona chakula kilicholetwa mezani mwake, jinsi maofisa walivyoketi mezani, jinsi watumishi walivyohudumu na walivyovalia, pia wanyweshaji wake na sadaka za kuteketezwa ambazo alizitoa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, aliduwaa na kushangaa mno.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
chakula kilichokuwa mezani pake, jinsi maafisa wake walivyokaa, wahudumu katika majoho yao, wanyweshaji wake na sadaka za kuteketezwa alizotoa katika Hekalu la Mwenyezi Mungu, alipatwa na mshangao mkubwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na chakula cha mezani pake, na watumishi wake walivyokaa, na kusimamia kwao wangoje wake, na mavazi yao, na wanyweshaji wake, na daraja yake ya kupandia mpaka nyumba ya Bwana, roho yake ilizimia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
tena alipoona chakula kilicholetwa mezani mwake, jinsi maofisa walivyoketi mezani, jinsi watumishi walivyohudumu na walivyovalia, pia wanyweshaji wake na sadaka za kuteketezwa ambazo alizitoa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, aliduwaa na kushangaa mno.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
chakula kilichokuwa mezani pake, jinsi maafisa wake walivyokaa, wahudumu katika majoho yao, wanyweshaji wake na sadaka za kuteketezwa alizotoa katika Hekalu la BWANA, alipatwa na mshangao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
chakula kilichokuwa mezani pake, jinsi maafisa wake walivyokaa, wahudumu katika majoho yao, wanyweshaji wake na sadaka za kuteketezwa alizotoa katika hekalu la bwana, alipatwa na mshangao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na chakula cha mezani pake, na maofisa wake walivyokaa, na kuhudumu kwao wahudumu wake, na mavazi yao, na wanyweshaji wake, na sadaka zake za kuteketezwa ambazo alizitoa katika nyumba ya BWANA, roho yake ilizimia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
tena alipoona chakula kilicholetwa mezani mwake, jinsi maofisa walivyoketi mezani, jinsi watumishi walivyohudumu na walivyovalia, pia wanyweshaji wake na sadaka za kuteketezwa ambazo alizitoa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, aliduwaa na kushangaa mno.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
aliyoijenga, na vilaji vilivyopo mezani na vikao vya watumwa wake na kazi za watumishi wake na mavazi yao na watunza vinywaji wake na ng'ombe zake za tambiko za kuteketezwa nzima, alizozipeleka Nyumbani mwa Bwana, ndipo, roho yake ilipozimia,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na chakula cha mezani pake, na watumishi wake walivyokaa, na kusimamia kwao wangoje wake, na mavazi yao, na wanyweshaji wake, na daraja yake ya kupandia mpaka nyumba ya BWANA, roho yake ilizimia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
tena alipoona chakula kilicholetwa kwa meza yake, jinsi wakubwa wake walivyoikaa kwenye meza, jinsi watumishi walivyotumika na walivyovaa, vilevile wenye kuleta vinywaji na sadaka za kuteketezwa ambazo alizitoa katika nyumba ya Yawe, alipumbazika na kushangaa sana.