1 Kings 11:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati Daudi alipowaangamiza Waedomu Yoabu, mkuu wa jeshi la Daudi, alikwenda huko kuwazika waliouawa. Yoabu aliwaua wanaume wote wa Edomu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hapo awali Daudi alipokuwa akipigana na Edomu, Yoabu jemadari wa jeshi, aliyekuwa ameenda kuzika waliouawa, alikuwa amewaua wanaume wote katika Edomu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana ikawa, Daudi alipokuwako Edomu, naye Yoabu, mkuu wa jeshi, amepanda awazike waliouawa, akiisha kumpiga kila mwanamume wa Edomu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati Daudi alipowaangamiza Waedomu Yoabu, mkuu wa jeshi la Daudi, alikwenda huko kuwazika waliouawa. Yoabu aliwaua wanaume wote wa Edomu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huko nyuma wakati Daudi alipokuwa akipigana na Edomu, Yoabu jemadari wa jeshi, aliyekuwa amekwenda kuzika waliouawa, alikuwa amewaua wanaume wote waliokuwako Edomu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huko nyuma wakati Daudi alipokuwa akipigana na Edomu, Yoabu jemadari wa jeshi, aliyekuwa amekwenda kuzika waliouawa, alikuwa amewaua wanaume wote waliokuwako Edomu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, Daudi alipokuwako Edomu, naye Yoabu, mkuu wa jeshi, amepanda awazike waliouawa, akiisha kumpiga kila mwanamume wa Edomu,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati Daudi alipowaangamiza Waedomu Yoabu, mkuu wa jeshi la Daudi, alikwenda huko kuwazika waliouawa. Yoabu aliwaua wanaume wote wa Edomu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ilikuwa siku zile, Dawidi alipowashinda Waedomu; hapo Yoabu, mkuu wa vikosi, alipanda kuwazika waliouawa. Ndipo, alipomwua kila mtu wa kiume aliyepatikana kule Edomu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana ikawa, Daudi alipokuwako Edomu, naye Yoabu, mkuu wa jeshi, amepanda awazike waliouawa, akiisha kumpiga kila mwanamume wa Edomu,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati Daudi alipowaangamiza Waedomu, Yoabu, jemadari wa waaskari wa Daudi, alikwenda kule kuwazika waliouawa. Yoabu aliwaua wanaume wote wa Edomu.