1 Kings 11:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hadadi na wenzake walisafiri kutoka Midiani, wakawachukua watu wengine huko Parani, wakaenda nao mpaka Misri, kwa Farao mfalme wa nchi hiyo. Farao akampatia Hadadi nyumba, akaamuru awe akipewa chakula, akampa na ardhi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakatoka Midiani wakaenda hadi Parani. Wakawachukua watu kutoka Parani, wakaenda nao Misri kwa Farao, mfalme wa Misri, ambaye alimpa Hadadi nyumba na shamba, na pia chakula.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaondoka katika Midiani, wakafika Parani; wakachukua pamoja nao watu toka Parani, wakafika Misri, kwa Farao mfalme wa Misri; aliyempa nyumba, akamwamria vyakula, akampa mashamba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hadadi na wenzake walisafiri kutoka Midiani, wakawachukua watu wengine huko Parani, wakaenda nao mpaka Misri, kwa Farao mfalme wa nchi hiyo. Farao akampatia Hadadi nyumba, akaamuru awe akipewa chakula, akampa na ardhi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakaondoka Midiani wakaenda Parani. Basi wakichukua pamoja nao wanaume kutoka Parani, wakaenda Misri, kwa Farao mfalme wa Misri, ambaye alimpa Hadadi nyumba, ardhi na akampatia chakula.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakaondoka Midiani wakaenda Parani. Basi wakichukua pamoja nao wanaume kutoka Parani, wakaenda Misri, kwa Farao mfalme wa Misri, ambaye alimpa Hadadi nyumba, ardhi na akampatia chakula.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaondoka katika Midiani, wakafika Parani; wakachukua pamoja nao watu toka Parani, wakafika Misri, kwa Farao mfalme wa Misri; aliyempa nyumba, akaamuru apewe vyakula, akampa mashamba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hadadi na wenzake walisafiri kutoka Midiani, wakawachukua watu wengine huko Parani, wakaenda nao mpaka Misri, kwa Farao mfalme wa nchi hiyo. Farao akampatia Hadadi nyumba, akaamuru awe akipewa chakula, akampa na ardhi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakaondoka Midiani, wakaja Parani, wakachukua watu wengine kule Parani kwenda nao Misri, kisha wakafika Misri kwa Farao, mfalme wa Misri. Huyu akampa nyumba, akamwagizia chakula, akampa nayo mashamba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaondoka katika Midiani, wakafika Parani; wakachukua pamoja nao watu toka Parani, wakafika Misri, kwa Farao mfalme wa Misri; aliyempa nyumba, akamwamria vyakula, akampa mashamba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hadadi na wenzake walisafiri kutoka Midiani, wakawakamata watu wengine kule Parani, wakaenda nao mpaka Misri, kwa mufalme wa Misri. Yeye akamupatia Hadadi nyumba, shamba, na chakula.