1 Kings 11:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
wanawake wa mataifa ambayo Mwenyezi-Mungu alikuwa amewakataza Waisraeli akisema, “Msioe kwao wala wao wasioe kwenu kwa sababu wanawake hao watapotosha mioyo yenu ili muitumikie miungu yao.” Solomoni aliwapenda sana wanawake hao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walitoka katika mataifa ambayo Mwenyezi Mungu aliwaambia Waisraeli, “Msije mkaoana nao, kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu mgeukie miungu yao.” Hata hivyo, Sulemani akakaza kuwapenda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
wanawake wa mataifa ambayo Mwenyezi-Mungu alikuwa amewakataza Waisraeli akisema, “Msioe kwao wala wao wasioe kwenu kwa sababu wanawake hao watapotosha mioyo yenu ili muitumikie miungu yao.” Solomoni aliwapenda sana wanawake hao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakitoka katika mataifa ambayo BWANA aliwaambia Waisraeli, “Msije mkaoana nao, kwa hakika wataigeuza mioyo yenu mgeukie miungu yao.” Hata hivyo, Solomoni akakaza kuwapenda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walitoka katika mataifa ambayo bwana aliwaambia Waisraeli, “Msije mkaoana nao, kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu mgeukie miungu yao.” Hata hivyo, Sulemani akakaza kuwapenda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na wa mataifa BWANA aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
wanawake wa mataifa ambayo Mwenyezi-Mungu alikuwa amewakataza Waisraeli akisema, “Msioe kwao wala wao wasioe kwenu kwa sababu wanawake hao watapotosha mioyo yenu ili muitumikie miungu yao.” Solomoni aliwapenda sana wanawake hao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wote ni wa wamizimu wale, ambao Bwana aliwaagiza wana wa Isiraeli kwamba: Msiingie kwao, wala wao wasiingie kwenu! Kwani wataigeuza mioyo yenu, mwifuate miungu yao. Wao ndio, Salomo aliogandamana nao kwa kuwapenda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na wa mataifa BWANA aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
ni kusema wanawake wa mataifa ambayo Yawe alikuwa amewakataza Waisraeli akisema: “Musioe kwao wala wao wasioe kwenu kwa sababu wanawake hao watapotosha mioyo yenu kusudi muitumikie miungu yao.” Solomono aliwapenda sana wanawake hao.