1 Kings 11:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo dada wa Tapenesi akamzalia Hadadi mwana aliyeitwa Genubathi. Genubathi alilelewa na Tapenesi katika nyumba ya Farao, pamoja na wana wa mfalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huyo dada yake Tapenesi akamzalia Hadadi mwana aliyeitwa Genubathi, ambaye alilelewa na Tapenesi katika jumba la kifalme. Huko, Genubathi akaishi pamoja na watoto wa Farao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye huyo umbu la Tapenesi akamzalia Genubathi mwanawe, ambaye Tapenesi alimlea nyumbani mwa Farao; naye Genubathi akawako nyumbani mwa Farao pamoja na wana wa Farao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo dada wa Tapenesi akamzalia Hadadi mwana aliyeitwa Genubathi. Genubathi alilelewa na Tapenesi katika nyumba ya Farao, pamoja na wana wa mfalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huyo ndugu wa Tapenesi akamzalia mwana aliyeitwa Genubathi, ambaye alilelewa na Tapenesi katika jumba la kifalme. Huko Genubathi aliishi pamoja na watoto wa Farao mwenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huyo ndugu wa Tapenesi akamzalia mwana aliyeitwa Genubathi, ambaye alilelewa na Tapenesi katika jumba la kifalme. Huko Genubathi aliishi pamoja na watoto wa Farao mwenyewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye huyo dada ya Tapanesi akamzalia Genubathi mwanawe, ambaye Tapanesi alimlea nyumbani mwa Farao; naye Genubathi akawako nyumbani mwa Farao pamoja na wana wa Farao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo dada wa Tapenesi akamzalia Hadadi mwana aliyeitwa Genubathi. Genubathi alilelewa na Tapenesi katika nyumba ya Farao, pamoja na wana wa mfalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huyu ndugu ya Tahapenesi akamzalia mwana wa kiume, Genubati; naye Tahapenesi akamkuza nyumbani mwa Farao. Kwa hiyo Genubati alikuwa nyumbani mwa Farao katikati ya wanawe Farao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye huyo umbu la Tapenesi akamzalia Genubathi mwanawe, ambaye Tapenesi alimlea nyumbani mwa Farao; naye Genubathi akawako nyumbani mwa Farao pamoja na wana wa Farao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Huyo dada ya Tapanesi akamuzalia Hadadi mwana aliyeitwa Genubati. Genubati alilelewa na Tapanesi katika nyumba ya mufalme wa Misri, pamoja na wana wa mufalme.