1 Kings 11:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Rezoni alikuwa adui wa Israeli siku zote za utawala wa Solomoni, akamsumbua sana Solomoni kama naye Hadadi alivyomsumbua. Basi, Rezoni aliidharau Israeli, naye alitawala nchi ya Aramu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Rezoni alikuwa adui wa Israeli kwa muda wote alioishi Sulemani, kuongezea matatizo yaliyosababishwa na Hadadi. Kwa hiyo Rezoni akatawala katika Aramu na akawa mkatili kwa Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akawa adui wa Israeli siku zote za Sulemani, zaidi ya madhara yake Hadadi; naye akawachukia Israeli, akamiliki juu ya Shamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Rezoni alikuwa adui wa Israeli siku zote za utawala wa Solomoni, akamsumbua sana Solomoni kama naye Hadadi alivyomsumbua. Basi, Rezoni aliidharau Israeli, naye alitawala nchi ya Aramu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Rezoni alikuwa adui wa Israeli kwa muda wote alioishi Solomoni, ukiongezea matatizo yaliyosababishwa na Hadadi. Kwa hiyo Rezoni akatawala katika Aramu na alikuwa mkatili kwa Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Rezoni alikuwa adui wa Israeli kwa muda wote alioishi Sulemani, ukiongezea matatizo yaliyosababishwa na Hadadi. Kwa hiyo Rezoni akatawala katika Aramu na alikuwa mkatili kwa Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye akawa adui wa Israeli siku zote za Sulemani, zaidi ya madhara yake Hadadi; naye akawachukia Israeli, akamiliki juu ya Shamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Rezoni alikuwa adui wa Israeli siku zote za utawala wa Solomoni, akamsumbua sana Solomoni kama naye Hadadi alivyomsumbua. Basi, Rezoni aliidharau Israeli, naye alitawala nchi ya Aramu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawa mpingani wa Waisiraeli siku zote za maisha yake Salomo. Akayaongeza yale mabaya, Hadadi aliyoyafanya, akachukizwa na Waisiraeli, akawa mfalme wa Ushami.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akawa adui wa Israeli siku zote za Sulemani, zaidi ya madhara yake Hadadi; naye akawachukia Israeli, akamiliki juu ya Shamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Resoni alikuwa adui wa Waisraeli siku zote za utawala wa Solomono, akamusumbua sana Solomono kama naye Hadadi alivyomusumbua. Basi, Resoni aliizarau inchi ya Israeli, naye alitawala inchi ya Aramu.