1 Kings 11:26 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeroboamu mwana wa Nebati, Mwefraimu wa Sereda, mtumishi wa Solomoni, ambaye mama yake mjane, aliitwa Zerua, pia alimwasi mfalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia, Yeroboamu mwana wa Nebati aliasi dhidi ya mfalme. Alikuwa mmoja wa maafisa wa Sulemani, Mwefraimu kutoka Sereda, ambaye mama yake alikuwa mjane aliyeitwa Serua.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Yeroboamu wa Nebati, Mwefraimu wa Sereda, mtumwa wake Sulemani; ambaye jina lake mamaye aliitwa Serua, mwanamke aliyefiwa na mumewe; yeye naye akainua mkono wake juu ya mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeroboamu mwana wa Nebati, Mwefraimu wa Sereda, mtumishi wa Solomoni, ambaye mama yake mjane, aliitwa Zerua, pia alimwasi mfalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia, Yeroboamu mwana wa Nebati aliasi dhidi ya mfalme. Alikuwa mmoja wa maafisa wa Solomoni, Mwefraimu kutoka Sereda, ambaye mama yake alikuwa mjane aliyeitwa Serua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia, Yeroboamu mwana wa Nebati aliasi dhidi ya mfalme. Alikuwa mmoja wa maafisa wa Sulemani, Mwefraimu kutoka Sereda, ambaye mama yake alikuwa mjane aliyeitwa Serua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Yeroboamu wa Nebati, Mwefraimu wa Sereda, mtumwa wake Sulemani; ambaye jina lake mamaye aliitwa Serua, mwanamke aliyefiwa na mumewe; yeye naye akamwasi mfalme.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeroboamu mwana wa Nebati, Mwefraimu wa Sereda, mtumishi wa Solomoni, ambaye mama yake mjane, aliitwa Zerua, pia alimwasi mfalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alikuwako naye Yeroboamu, mwana wa Nebati wa Efuraimu wa mji wa Sereda; jina la mama yake ni Serua aliyekuwa mjane. Yeroboamu alikuwa mtumishi wa Salomo, lakini aliinua mkono kwa kumkataa mfalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Yeroboamu wa Nebati, Mwefraimu wa Sereda, mtumwa wake Sulemani; ambaye jina lake mamaye aliitwa Serua, mwanamke aliyefiwa na mumewe; yeye naye akainua mkono wake juu ya mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yeroboamu mwana wa Nebati Mwefuraimu wa muji wa Zereda, mutumishi wa Solomono, ambaye mama yake mujane aliitwa Zerua, naye alimwasi mufalme.