1 Kings 11:31 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
halafu akamwambia Yeroboamu, “Jitwalie vipande kumi maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, asema hivi: ‘Tazama, karibu nitaurarua ufalme na kuuondoa mikononi mwa Solomoni, nami nitakupa wewe makabila kumi.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha akamwambia Yeroboamu, “Jichukulie vipande kumi, kwa kuwa hivi ndivyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, asemavyo: ‘Tazama, ninaenda kumnyang’anya Sulemani ufalme na kukupa makabila kumi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamwambia Yeroboamu, Twaa wewe vipande kumi, maana Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nitaurarua ufalme, na kuuondoa katika mkono wa Sulemani, nami nitakupa wewe kabila kumi,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
halafu akamwambia Yeroboamu, “Jitwalie vipande kumi maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, asema hivi: ‘Tazama, karibu nitaurarua ufalme na kuuondoa mikononi mwa Solomoni, nami nitakupa wewe makabila kumi.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akamwambia Yeroboamu, “Chukua vipande kumi kwa ajili yako, kwa kuwa hivi ndivyo BWANA, Mungu wa Israeli asemavyo: ‘Tazama, ninakwenda kuuchana ufalme kutoka mikononi mwa Solomoni na kukupa wewe makabila kumi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha akamwambia Yeroboamu, “Chukua vipande kumi kwa ajili yako, kwa kuwa hivi ndivyo bwana, Mungu wa Israeli asemavyo: ‘Tazama, ninakwenda kuuchana ufalme kutoka mikononi mwa Sulemani na kukupa wewe makabila kumi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamwambia Yeroboamu, Twaa wewe vipande kumi, maana BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nitaurarua ufalme, na kuuondoa katika mkono wa Sulemani, nami nitakupa wewe makabila kumi,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
halafu akamwambia Yeroboamu, “Jitwalie vipande kumi maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, asema hivi: ‘Tazama, karibu nitaurarua ufalme na kuuondoa mikononi mwa Solomoni, nami nitakupa wewe makabila kumi.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akamwambia Yeroboamu: Jitwalie vipande kumi! Kwani ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyokuambia: Utaniona, nikimnyang'anya Salomo ufalme mkononi mwake, nikupe wewe mashina kumi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamwambia Yeroboamu, Twaa wewe vipande kumi, maana BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nitaurarua ufalme, na kuuondoa katika mkono wa Sulemani, nami nitakupa wewe kabila kumi,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
halafu akamwambia Yeroboamu: “Ujitwalie vipande kumi maana Yawe, Mungu wa Israeli, anasema: ‘Sasa hivi nitaurarua ufalme na kuuondoa katika mikono ya Solomono, nami nitakupa wewe makabila kumi.