1 Kings 11:34 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata hivyo, sitamnyanganya milki yote, wala sitamwondolea mamlaka maishani mwake, kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi ambaye nilimchagua, na ambaye alifuata amri zangu na maongozi yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Lakini sitauondoa ufalme wote mkononi mwa Sulemani; nimemfanya mtawala siku zote za maisha yake kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, niliyemchagua na ambaye aliyatunza maagizo na amri zangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walakini sitauondoa ufalme wote katika mkono wake; lakini nitamfanya awe mkuu siku zote za maisha yake, kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi niliyemchagua kwa maana alizishika amri zangu na sheria zangu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata hivyo, sitamnyang'anya milki yote, wala sitamwondolea mamlaka maishani mwake, kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi ambaye nilimchagua, na ambaye alifuata amri zangu na maongozi yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Lakini sitauondoa ufalme wote kutoka mikononi mwa Solomoni, nimemfanya mtawala siku zote za maisha yake kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, niliyemchagua na ambaye aliyatunza maagizo na amri zangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Lakini sitauondoa ufalme wote kutoka mikononi mwa Sulemani, nimemfanya mtawala siku zote za maisha yake kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, niliyemchagua na ambaye aliyatunza maagizo na amri zangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini sitauondoa ufalme wote katika mkono wake; bali nitamfanya awe mkuu siku zote za maisha yake, kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi niliyemchagua kwa maana alizishika amri zangu na sheria zangu,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata hivyo, sitamnyanganya milki yote, wala sitamwondolea mamlaka maishani mwake, kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi ambaye nilimchagua, na ambaye alifuata amri zangu na maongozi yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini sitauondoa ufalme wote mkononi mwake yeye, ila nitamweka kuwa mkuu siku zote za maisha yake kwa ajili ya mtumishi wangu Dawidi, niliyemchagua, aliyeyaangalia maagizo yangu na maongozi yangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walakini sitauondoa ufalme wote katika mkono wake; lakini nitamfanya awe mkuu siku zote za maisha yake, kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi niliyemchagua kwa maana alizishika amri zangu na sheria zangu,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hata hivyo, sitamunyanganya urizi wote, wala sitamwondolea mamlaka wakati angali anaishi, kwa ajili ya mutumishi wangu Daudi ambaye nilimuchagua, na ambaye alifuata amri zangu na masharti yangu.