1 Kings 11:36 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo mwanawe Solomoni nitamwachia kabila moja, ili wakati wote mzawa wa mtumishi wangu Daudi awe anatawala Yerusalemu, awe taa inayoangaza daima mbele yangu katika mji ambao nimeuchagua uwe mahali pa kuniabudia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitampa mwanawe kabila moja ili Daudi mtumishi wangu awe na taa mbele zangu daima katika Yerusalemu, mji ambao nimeuchagua kuweka Jina langu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitampa mwana wake kabila moja, ili Daudi, mtumishi wangu, apate kuwa na taa siku zote mbele zangu katika Yerusalemu, mji ule niliouchagua niweke jina langu huko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo mwanawe Solomoni nitamwachia kabila moja, ili wakati wote mzawa wa mtumishi wangu Daudi awe anatawala Yerusalemu, awe taa inayoangaza daima mbele yangu katika mji ambao nimeuchagua uwe mahali pa kuniabudia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitampa mwanawe kabila moja ili kwamba Daudi mtumishi wangu awe na taa mbele zangu daima katika Yerusalemu, mji ambao nimeuchagua kuweka Jina langu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitampa mwanawe kabila moja ili kwamba Daudi mtumishi wangu awe na taa mbele zangu daima katika Yerusalemu, mji ambao nimeuchagua kuweka Jina langu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitampa mwana wake kabila moja, ili Daudi, mtumishi wangu, apate kuwa na taa siku zote mbele zangu katika Yerusalemu, mji ule niliouchagua niweke jina langu huko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo mwanawe Solomoni nitamwachia kabila moja, ili wakati wote mzawa wa mtumishi wangu Daudi awe anatawala Yerusalemu, awe taa inayoangaza daima mbele yangu katika mji ambao nimeuchagua uwe mahali pa kuniabudia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwanawe nitampa shina moja, kusudi mtumishi wangu Dawidi awe siku zote na taa iwakayo mbele yangu huko Yerusalemu, mle mjini, nilimochagua kuwa mwa kulikalishia humo Jina langu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitampa mwana wake kabila moja, ili Daudi, mtumishi wangu, apate kuwa na taa siku zote mbele zangu katika Yerusalemu, mji ule niliouchagua niweke jina langu huko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Huyo mwana wa Solomono nitamwachia kabila moja, kusudi wakati wote mutu mumoja wa uzao wa mutumishi wangu Daudi akuwe anatawala Yerusalema, akuwe taa inayoangaza siku zote mbele yangu katika muji ambao nimeuchagua ukuwe pahali pa kuniabudia.