1 Kings 12:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini watu wote wa Israeli walipoona kwamba mfalme hakuwajali, walimwambia, “Hatuna uhusiano wowote na Daudi! Hatuna sehemu yetu kutoka kwa huyo mwana wa Yese. Rudini nyumbani, enyi watu wa Israeli! Itunze nyumba yako mwenyewe, ee Daudi.” Hivyo, watu wa Israeli wakarudi makwao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Israeli wote walipoona kuwa mfalme amekataa kuwasikiliza, wakamjibu mfalme: “Je, tuna fungu gani kwa Daudi? Tuna urithi gani kwa mwana wa Yese? Nendeni kwenye mahema yenu, ee Israeli! Angalia nyumba yako mwenyewe, ee Daudi!” Hivyo Waisraeli wakaenda kwenye mahema yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Israeli wote walipoona ya kuwa mfalme hakuwasikia, hao watu walimjibu mfalme, wakasema, Tuna sehemu gani katika Daudi? Wala hatuna urithi katika mwana wa Yese. Haya! Nendeni zenu hemani kwenu, enyi Israeli; sasa itunze nyumba yako mwenyewe, Ee Daudi. Hivyo Israeli wakaenda zao hemani kwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini watu wote wa Israeli walipoona kwamba mfalme hakuwajali, walimwambia, “Hatuna uhusiano wowote na Daudi! Hatuna sehemu yetu kutoka kwa huyo mwana wa Yese. Rudini nyumbani, enyi watu wa Israeli! Itunze nyumba yako mwenyewe, ee Daudi.” Hivyo, watu wa Israeli wakarudi makwao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Israeli wote walipoona kuwa mfalme amekataa kuwasikiliza, wakamjibu mfalme: “Tuna fungu gani kwa Daudi? Sisi hatuna urithi kwa mwana wa Yese. Nendeni kwenye mahema yenu, Ee Israeli! Angalia nyumba yako mwenyewe, Ee Daudi!” Hivyo Waisraeli wakaenda kwenye mahema yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Israeli wote walipoona kuwa mfalme amekataa kuwasikiliza, wakamjibu mfalme: “Tuna fungu gani kwa Daudi? Sisi hatuna urithi kwa mwana wa Yese. Nendeni kwenye mahema yenu, ee Israeli! Angalia nyumba yako mwenyewe, ee Daudi!” Hivyo Waisraeli wakaenda kwenye mahema yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Israeli wote walipoona ya kuwa mfalme hakuwasikia, hao watu walimjibu mfalme, wakasema, Tuna sehemu gani katika Daudi? Wala hatuna urithi katika mwana wa Yese. Haya! Nendeni zenu hemani kwenu, enyi Israeli; sasa itunze nyumba yako mwenyewe, Ee Daudi. Hivyo Israeli wakaenda zao hemani kwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini watu wote wa Israeli walipoona kwamba mfalme hakuwajali, walimwambia, “Hatuna uhusiano wowote na Daudi! Hatuna sehemu yetu kutoka kwa huyo mwana wa Yese. Rudini nyumbani, enyi watu wa Israeli! Itunze nyumba yako mwenyewe, ee Daudi.” Hivyo, watu wa Israeli wakarudi makwao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waisiraeli wote walipoona, ya kuwa mfalme hakuwasikia, ndipo, watu walipomjibu mfalme neno la kwamba: Sisi tuna bia gani na Dawidi? Hatuna fungu lo lote kwake mwana wa Isai. Waisiraeli, haya! Rudini sasa mahemani kwenu! Nawe Dawidi, na uuangalie mwenyewe mlango wako! Ndipo, Waisiraeli walipokwenda mahemani kwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Israeli wote walipoona ya kuwa mfalme hakuwasikia, hao watu walimjibu mfalme, wakasema, Tuna sehemu gani katika Daudi? Wala hatuna urithi katika mwana wa Yese. Haya! Nendeni zenu hemani kwenu, enyi Israeli; sasa itunze nyumba yako mwenyewe, Ee Daudi. Hivyo Israeli wakaenda zao hemani kwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini watu wote wa Israeli walipoona kwamba mufalme hakuwajali, walimwambia: “Hatuna ushirika wowote na Daudi! Hatuna sehemu yetu kutoka kwa huyo mwana wa Yese. Murudie kwenu, enyi watu wa Israeli! Uitunze nyumba yako mwenyewe, ee Daudi.” Hivyo, watu wa Israeli wakarudi kila mutu kwake.