1 Kings 12:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Rehoboamu alipofika Yerusalemu, alikusanya askari stadi 180,000 wa makabila ya Yuda na Benyamini, apate kupigana na utawala wa Israeli, ili aurudishe utawala kwake yeye mwenyewe Rehoboamu, mwana wa Solomoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba yote ya Yuda na kabila la Benyamini, vijana wenye uwezo elfu mia moja na themanini, ili kufanya vita dhidi ya nyumba ya Israeli na kuurudisha ufalme kwa Rehoboamu mwana wa Sulemani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba yote ya Yuda, pamoja na kabila ya Benyamini, watu wateule mia na themanini elfu, waliokuwa watu wa vita, ili wapigane na nyumba ya Israeli, waurudishe ufalme tena kwa Rehoboamu mwana wa Sulemani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Rehoboamu alipofika Yerusalemu, alikusanya askari stadi 180,000 wa makabila ya Yuda na Benyamini, apate kupigana na utawala wa Israeli, ili aurudishe utawala kwake yeye mwenyewe Rehoboamu, mwana wa Solomoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikawa Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba yote ya Yuda na kabila la Benyamini, wanaume wapiganaji 180,000, kufanya vita dhidi ya nyumba ya Israeli na kuurudisha tena ufalme kwa Rehoboamu mwana wa Solomoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikawa Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba yote ya Yuda na kabila la Benyamini, wanaume wapiganaji 180,000, kufanya vita dhidi ya nyumba ya Israeli na kuurudisha tena ufalme kwa Rehoboamu mwana wa Sulemani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba yote ya Yuda, pamoja na kabila la Benyamini, watu wateule elfu mia moja themanini, waliokuwa watu wa vita, ili wapigane na nyumba ya Israeli, waurudishe ufalme tena kwa Rehoboamu mwana wa Sulemani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Rehoboamu alipofika Yerusalemu, alikusanya askari stadi 180,000 wa makabila ya Yuda na Benyamini, apate kupigana na utawala wa Israeli, ili aurudishe utawala kwake yeye mwenyewe Rehoboamu, mwana wa Solomoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Rehabeamu alipofika Yerusalemu akaukusanya mlango wote wa Yuda na shina la Benyamini, watu 180000 waliochaguliwa kupiga vita, wapigane na mlango wa Waisiraeli, wamrudishie Rehabeamu, mwana wa Salomo, ufalme huo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba yote ya Yuda, pamoja na kabila ya Benyamini, watu wateule mia na themanini elfu, waliokuwa watu wa vita, ili wapigane na nyumba ya Israeli, waurudishe ufalme tena kwa Rehoboamu mwana wa Sulemani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Rehoboamu alipofika Yerusalema, alikusanya waaskari wafundi wa vita elfu mia moja na makumi nane wa makabila ya Yuda na Benjamina, apate kupigana na utawala wa Israeli, kusudi aurudishe utawala kwa Rehoboamu mwana wa Solomono.