1 Kings 13:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo mzee wa Betheli akamwambia, “Mimi pia ni nabii kama wewe, na Mwenyezi-Mungu amenena nami kwa njia ya malaika akisema, ‘Mrudishe nyumbani kwako, ale chakula na kunywa maji.’” Lakini huyo nabii mzee alikuwa anamdanganya tu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule nabii mzee akajibu, “Mimi pia ni nabii, kama wewe. Naye malaika alisema nami kwa neno la Mwenyezi Mungu: ‘Mrudishe aje katika nyumba yako ili apate kula mkate na kunywa maji.’ ” (Lakini alikuwa akimwambia uongo.)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamwambia, Mimi nami ni nabii kama wewe, na malaika akaniambia kwa neno la Bwana, kusema, Mrudishe pamoja nawe nyumbani kwako, ale chakula, akanywe maji. Lakini alisema uongo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo mzee wa Betheli akamwambia, “Mimi pia ni nabii kama wewe, na Mwenyezi-Mungu amenena nami kwa njia ya malaika akisema, ‘Mrudishe nyumbani kwako, ale chakula na kunywa maji.’” Lakini huyo nabii mzee alikuwa anamdanganya tu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule nabii mzee akajibu, “Mimi pia ni nabii, kama wewe. Naye malaika alisema nami kwa neno la BWANA: ‘Mrudishe aje katika nyumba yako ili apate kula mkate na kunywa maji.’ ” (Lakini alikuwa akimwambia uongo.)
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule nabii mzee akajibu, “Mimi pia ni nabii, kama wewe. Naye malaika alisema nami kwa neno la bwana: ‘Mrudishe aje katika nyumba yako ili apate kula mkate na kunywa maji.’ ” (Lakini alikuwa akimwambia uongo.)
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamwambia, Mimi nami ni nabii kama wewe, na malaika kaniambia kwa neno la BWANA, kusema, Mrudishe pamoja nawe nyumbani kwako, ale chakula, akanywe maji. Lakini alisema uongo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo mzee wa Betheli akamwambia, “Mimi pia ni nabii kama wewe, na Mwenyezi-Mungu amenena nami kwa njia ya malaika akisema, ‘Mrudishe nyumbani kwako, ale chakula na kunywa maji.’” Lakini huyo nabii mzee alikuwa anamdanganya tu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, yule alipomwambia: Mimi mami ni mfumbuaji kama wewe; nami malaika ameniambia kwa kuagizwa na Bwana kwamba: Umrudishe kwako nyumbani, ale chakula, anywe maji! Lakini huko alimwongopea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamwambia, Mimi nami ni nabii kama wewe, na malaika akaniambia kwa neno la BWANA, kusema, Mrudishe pamoja nawe nyumbani kwako, ale chakula, akanywe maji. Lakini alisema uongo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule muzee wa Beteli akamwambia: “Mimi vilevile ni nabii kama wewe, na Yawe amesema nami kwa njia ya malaika akisema: ‘Umurudishe kwako, akule chakula na kunywa maji.’ ” Lakini yule nabii muzee alikuwa anamudanganya tu.