1 Kings 13:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu huyo akailaani ile madhabahu akisema, “Ee madhabahu! Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Atazaliwa mtoto katika ukoo wa Daudi, jina lake Yosia. Huyo atawatwaa makuhani wanaohudumu mahali pa ibada na kufukiza ubani juu yako, na kutambika juu yako; naam, mifupa ya watu itateketezwa juu yako!’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akapiga kelele dhidi ya madhabahu kwa neno la Mwenyezi Mungu: “Ee madhabahu, ee madhabahu! Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: ‘Mwana aitwaye Yosia atazaliwa katika nyumba ya Daudi. Juu yako atawatoa dhabihu makuhani wa mahali pa juu pa kuabudia ambao hutoa sadaka hapa, nayo mifupa ya wanadamu itateketezwa juu yako.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mtu huyo akapiga kelele juu ya madhabahu, kwa neno la Bwana akasema, Ee madhabahu, madhabahu, Bwana asema hivi, Angalia, mtoto atazaliwa katika nyumba ya Daudi, jina lake Yosia; na juu yako atawachinja makuhani wa mahali pa juu, wanaofukiza uvumba juu yako, na mifupa ya watu itateketezwa juu yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu huyo akailaani ile madhabahu akisema, “Ee madhabahu! Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Atazaliwa mtoto katika ukoo wa Daudi, jina lake Yosia. Huyo atawatwaa makuhani wanaohudumu mahali pa ibada na kufukiza ubani juu yako, na kutambika juu yako; naam, mifupa ya watu itateketezwa juu yako!’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akapiga kelele dhidi ya madhabahu kwa neno la BWANA: “Ee madhabahu, madhabahu! Hivi ndivyo asemavyo BWANA: ‘Mwana aitwaye Yosia atazaliwa katika nyumba ya Daudi. Juu yako atawatoa dhabihu makuhani wa mahali pa juu pa kuabudia miungu wale ambao wanatoa sadaka hapa sasa, nayo mifupa ya wanadamu itachomwa juu yako.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akapiga kelele dhidi ya madhabahu kwa neno la bwana: “Ee madhabahu, madhabahu! Hivi ndivyo asemavyo bwana: ‘Mwana aitwaye Yosia atazaliwa katika nyumba ya Daudi. Juu yako atawatoa dhabihu makuhani wa mahali pa juu pa kuabudia miungu wale ambao wanatoa sadaka hapa sasa, nayo mifupa ya wanadamu itachomwa juu yako.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi mtu huyo akapiga kelele juu ya madhabahu, kwa neno la BWANA akasema, Ee madhabahu, madhabahu, BWANA asema hivi, Angalia, mtoto atazaliwa katika nyumba ya Daudi, jina lake Yosia; na juu yako atawachinja makuhani wa mahali pa juu, wanaofukiza uvumba juu yako, na mifupa ya watu itateketezwa juu yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu huyo akailaani ile madhabahu akisema, “Ee madhabahu! Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Atazaliwa mtoto katika ukoo wa Daudi, jina lake Yosia. Huyo atawatwaa makuhani wanaohudumu mahali pa ibada na kufukiza ubani juu yako, na kutambika juu yako; naam, mifupa ya watu itateketezwa juu yako!’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa kuagizwa na Bwana akapaza sauti kwa ajili ya hiyo meza ya kutambikia, akasema: Meza ya kutambikia! Meza ya kutambikia! Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Tazama! Nyumbani mwa Dawidi atazaliwa mwana, jina lake Yosia; yeye atachinja juu yako kuwa ng'ombe za tambiko watambikaji wa vijumba vya vilimani wanaovukiza juu yako; ndipo, watakapoteketeza juu yako mifupa ya watu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mtu huyo akapiga kelele juu ya madhabahu, kwa neno la BWANA akasema, Ee madhabahu, madhabahu, BWANA asema hivi, Angalia, mtoto atazaliwa katika nyumba ya Daudi, jina lake Yosia; na juu yako atawachinja makuhani wa mahali pa juu, wanaofukiza uvumba juu yako, na mifupa ya watu itateketezwa juu yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu huyo akailaani ile mazabahu akisema: “Ee mazabahu, Yawe anasema hivi: ‘Kutazaliwa mutoto katika ukoo wa Daudi, jina lake Yosia. Huyo atawatwaa makuhani wanaotumika kwa nafasi ya ibada na kufukiza ubani juu yako, na kuwatambika juu yako. Hakika, mifupa ya watu itateketezwa juu yako!’ ”