1 Kings 13:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu waliopitia hapo na kuiona maiti barabarani, na simba amesimama karibu nayo, wakaenda mpaka mjini alimokuwa anakaa yule nabii, wakawaambia watu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu waliopita pale, waliona maiti iliyokuwa imebwagwa, simba akiwa amesimama kando yake. Nao wakaenda kutoa habari katika mji ambao nabii mzee alikuwa anaishi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tazama, watu wakapita, wakauona mzoga umetupwa njiani, na yule simba akisimama karibu na mzoga, wakaenda, wakatoa habari katika mji ule alimokaa yule nabii mzee.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu waliopitia hapo na kuiona maiti barabarani, na simba amesimama karibu nayo, wakaenda mpaka mjini alimokuwa anakaa yule nabii, wakawaambia watu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baadhi ya watu waliopita pale waliona maiti imebwagwa pale chini, simba akiwa amesimama kando ya maiti, wakaenda na kutoa habari katika mji ambao nabii mzee aliishi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baadhi ya watu waliopita pale waliona maiti imebwagwa pale chini, simba akiwa amesimama kando ya maiti, wakaenda na kutoa habari katika mji ambao nabii mzee aliishi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tazama, watu wakapita, wakauona mzoga umetupwa njiani, na yule simba akisimama karibu na mzoga, wakaenda, wakatoa habari katika mji ule alimokaa yule nabii mzee.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu waliopitia hapo na kuiona maiti barabarani, na simba amesimama karibu nayo, wakaenda mpaka mjini alimokuwa anakaa yule nabii, wakawaambia watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mara watu waliopita wakaiona maiti, ilivyolala njiani, naye simba aliyesimama kando yake maiti, wakaja, wakayasimulia mle mjini, yule mfumbuaji mzee alimokaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tazama, watu wakapita, wakauona mzoga umetupwa njiani, na yule simba akisimama karibu na mzoga, wakaenda, wakatoa habari katika mji ule alimokaa yule nabii mzee.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu waliopitia pale na kuiona maiti katika barabara, na simba akisimama karibu nayo, wakaenda mpaka katika muji yule nabii alimokuwa anakaa, wakawaambia watu.