1 Kings 13:32 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mambo yote aliyoagizwa na Mwenyezi-Mungu dhidi ya madhabahu ya Betheli, na mahali pote pa kutambikia vilimani Samaria, hakika yatatimia.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana ujumbe alioutangaza kwa neno la Mwenyezi Mungu dhidi ya madhabahu huko Betheli, na dhidi ya nyumba zote za ibada katika mahali pa juu pa kuabudia ndani ya miji ya Samaria, hakika utatimia.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana neno hilo alilolia juu ya madhabahu katika Betheli, kwa neno la Bwana, na juu ya nyumba zote za mahali pa juu zilizo katika miji ya Samaria, hakika litatimizwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mambo yote aliyoagizwa na Mwenyezi-Mungu dhidi ya madhabahu ya Betheli, na mahali pote pa kutambikia vilimani Samaria, hakika yatatimia.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana ujumbe alioutangaza kwa neno la BWANA dhidi ya madhabahu huko Betheli na dhidi ya madhabahu yote katika mahali pa juu pa kuabudia miungu katika miji ya Samaria, hakika yatatokea kweli.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana ujumbe alioutangaza kwa neno la bwana dhidi ya madhabahu huko Betheli na dhidi ya madhabahu yote katika mahali pa juu pa kuabudia miungu katika miji ya Samaria, hakika yatatokea kweli.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana neno hilo alilolia juu ya madhabahu katika Betheli, kwa neno la BWANA, na juu ya nyumba zote za mahali pa juu zilizo katika miji ya Samaria, hakika litatimizwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mambo yote aliyoagizwa na Mwenyezi-Mungu dhidi ya madhabahu ya Betheli, na mahali pote pa kutambikia vilimani Samaria, hakika yatatimia.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani litatimia kweli lile neno, alilolisema na kupaza sauti kwa kuagizwa na Bwana kwa ajili ya meza ya kutambikia iliyoko Beteli na kwa ajili ya vijumba vyote vya kutambikia vilivyoko vilimani juu katika miji ya Samaria.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana neno hilo alilolia juu ya madhabahu katika Betheli, kwa neno la BWANA, na juu ya nyumba zote za mahali pa juu zilizo katika miji ya Samaria, hakika litatimizwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mambo yote aliyoagizwa na Yawe juu ya mazabahu ya Beteli, na nafasi yote ya kutambikia juu ya vilima vya Samaria, hakika yatatimia.”