1 Kings 13:33 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeroboamu hakuuacha upotovu wake; aliendelea kuteua watu wa kawaida kuwa makuhani, wahudumie mahali pa kutambikia vilimani. Mtu yeyote aliyejitolea, alimweka wakfu kuwa kuhani wa mahali pa kutambikia huko vilimani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata baada ya haya, Yeroboamu hakubadili njia zake mbaya, lakini mara nyingine tena akaweka makuhani kwa ajili ya mahali pa juu pa kuabudia kutoka watu wa aina zote. Yeyote aliyetaka kuwa kuhani alimweka wakfu kwa ajili ya mahali pa juu pa kuabudia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baada ya hayo Yeroboamu hakuiacha njia yake mbovu, lakini akafanya tena makuhani wa mahali pa juu, wa watu wo wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeroboamu hakuuacha upotovu wake; aliendelea kuteua watu wa kawaida kuwa makuhani, wahudumie mahali pa kutambikia vilimani. Mtu yeyote aliyejitolea, alimweka wakfu kuwa kuhani wa mahali pa kutambikia huko vilimani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata baada ya haya, Yeroboamu hakubadili njia zake mbaya, lakini mara nyingine tena akaweka makuhani kwa ajili ya mahali pa juu pa kuabudia miungu kutoka watu wa aina zote. Ye yote aliyetaka kuwa kuhani alimweka wakfu kwa ajili ya mahali pa juu pa kuabudia miungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata baada ya haya, Yeroboamu hakubadili njia zake mbaya, lakini mara nyingine tena akaweka makuhani kwa ajili ya mahali pa juu pa kuabudia miungu kutoka watu wa aina zote. Yeyote aliyetaka kuwa kuhani alimweka wakfu kwa ajili ya mahali pa juu pa kuabudia miungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baada ya hayo Yeroboamu hakuiacha njia yake mbovu, lakini akafanya tena makuhani wa mahali pa juu, wa watu wowote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeroboamu hakuuacha upotovu wake; aliendelea kuteua watu wa kawaida kuwa makuhani, wahudumie mahali pa kutambikia vilimani. Mtu yeyote aliyejitolea, alimweka wakfu kuwa kuhani wa mahali pa kutambikia huko vilimani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hayo yalipofanyika, Yeroboamu hakurudi na kuiacha njia yake mbaya, akaweka tena watu wo wote kuwa watambikaji wa vilimani; aliyependezwa naye akamjaza gao, awe mtambikaji wa vilimani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baada ya hayo Yeroboamu hakuiacha njia yake mbovu, lakini akafanya tena makuhani wa mahali pa juu, wa watu wo wote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yeroboamu hakuuacha upotovu wake; aliendelea kuchagua watu wa kawaida kuwa makuhani, watumike kwa nafasi ya kutambikia juu ya vilima. Mutu yeyote aliyejitolea, alimutakasa kuwa kuhani wa nafasi ya kutambikia kule juu ya vilima.