1 Kings 13:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Madhabahu nayo ikabomoka, na majivu yake yakamwagika chini, kama ishara ile aliyoitoa huyo mtu wa Mungu na ujumbe wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia, madhabahu yakapasuka na majivu yakamwagika, sawasawa na ishara iliyotolewa na mtu wa Mungu kwa neno la Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Madhabahu ikapasuka, majivu ya madhabahuni yakamwagika, sawasawa na ishara aliyoitoa mtu wa Mungu kwa neno la Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Madhabahu nayo ikabomoka, na majivu yake yakamwagika chini, kama ishara ile aliyoitoa huyo mtu wa Mungu na ujumbe wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia, madhabahu ilipasuka na majivu yakamwagika sawasawa na ishara iliyotolewa na mtu wa Mungu kwa neno la BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia, madhabahu yalipasuka na majivu yakamwagika sawasawa na ishara iliyotolewa na mtu wa Mungu kwa neno la bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Madhabahu ikapasuka, majivu ya madhabahuni yakamwagika, sawasawa na ishara aliyoitoa mtu wa Mungu kwa neno la BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Madhabahu nayo ikabomoka, na majivu yake yakamwagika chini, kama ishara ile aliyoitoa huyo mtu wa Mungu na ujumbe wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo meza ya kutambikia ikapasuka, nayo majivu ya mafuta yaliyokuwa juu yake yakamwagika hapo mezani pa kutambikia; ndicho kielekezo, yule mtu wa Mungu alichowapa kwa kuagizwa na Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Madhabahu ikapasuka, majivu ya madhabahuni yakamwagika, sawasawa na ishara aliyoitoa mtu wa Mungu kwa neno la BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mazabahu nayo ikabomoka, na majivu yake yakamwangika chini, kama kitambulisho kile yule mutu wa Mungu alichokitoa na ujumbe wa Yawe.