1 Kings 14:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wote wa Israeli watafanya matanga na kumzika. Walakini, ni huyo tu wa jamaa ya Yeroboamu atakayezikwa, kwani ni yeye tu wa jamaa ya Yeroboamu aliyepata kumpendeza Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Israeli yote itamwombolezea na kumzika. Ni yeye pekee wa nyumba ya Yeroboamu atakayezikwa, kwa sababu ni yeye tu ndani ya nyumba ya Yeroboamu ambaye Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, ameona kitu chema kwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Israeli wote watamlilia, na kumzika, kwa maana ndiye peke yake wa Yeroboamu atakayeingia kaburini; kwa sababu limeonekana ndani yake jambo lililo jema kwa Bwana, Mungu wa Israeli, nyumbani mwa Yeroboamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wote wa Israeli watafanya matanga na kumzika. Walakini, ni huyo tu wa jamaa ya Yeroboamu atakayezikwa, kwani ni yeye tu wa jamaa ya Yeroboamu aliyepata kumpendeza Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Israeli yote itamwombolezea na kumzika. Kwa sababu ni yeye pekee wa nyumba ya Yeroboamu atakayezikwa, kwa sababu ni yeye peke yake ndani ya nyumba ya Yeroboamu ambaye BWANA, Mungu wa Israeli, ameona walau kitu cho chote chema kwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Israeli yote itamwombolezea na kumzika. Kwa sababu ni yeye pekee wa nyumba ya Yeroboamu atakayezikwa, kwa sababu ni yeye peke yake ndani ya nyumba ya Yeroboamu ambaye bwana, Mungu wa Israeli, ameona kitu chema kwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Israeli wote watamlilia, na kumzika, kwa maana ndiye peke yake wa Yeroboamu atakayeingia kaburini; kwa sababu limeonekana ndani yake jambo lililo jema kwa BWANA, Mungu wa Israeli, nyumbani mwa Yeroboamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wote wa Israeli watafanya matanga na kumzika. Walakini, ni huyo tu wa jamaa ya Yeroboamu atakayezikwa, kwani ni yeye tu wa jamaa ya Yeroboamu aliyepata kumpendeza Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waisiraeli wote watamwombolezea, kisha watamzika, kwani kwao wa Yeroboamu huyu peke yake ndiye atakayeingia kaburini, kwani katika mlango wa Yeroboamu ni kwake tu kulikoonekana yaliyokuwa mema machoni pa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Israeli wote watamlilia, na kumzika, kwa maana ndiye peke yake wa Yeroboamu atakayeingia kaburini; kwa sababu limeonekana ndani yake jambo lililo jema kwa BWANA, Mungu wa Israeli, nyumbani mwa Yeroboamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wote wa Israeli watafanya kilio na kumuzika. Lakini, ni huyo tu wa jamaa ya Yeroboamu atakayezikwa, maana ni yeye tu wa jamaa ya Yeroboamu aliyepata kupendezwa na Yawe, Mungu wa Israeli.