1 Kings 14:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naam, tangu sasa, Mwenyezi-Mungu atawapiga watu wa Israeli, nao watatikisika kama unyasi unavyotikiswa mtoni. Atawangoa kutoka nchi hii nzuri aliyowapa babu zao, na kuwatawanya mbali, ngambo ya mto Eufrate, kwa sababu wamemkasirisha Mwenyezi-Mungu kwa kujitengenezea sanamu za Ashera, mungu wa kike.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye Mwenyezi Mungu ataipiga Israeli, hata iwe kama mwanzi unaoyumbayumba kwenye maji. Ataing’oa Israeli kutoka nchi hii nzuri aliyowapa baba zao na kuwatawanya ng’ambo ya Mto, kwa sababu wamemghadhibisha Mwenyezi Mungu kwa kutengeneza nguzo za Ashera.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa Bwana atawapiga Israeli kama manyasi yatikiswavyo majini; naye atawang'oa Israeli katika nchi hii njema, aliyowapa baba zao, naye atawatawanya ng'ambo ya Mto; kwa sababu wamejifanyia maashera yao, wakimkasirisha Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naam, tangu sasa, Mwenyezi-Mungu atawapiga watu wa Israeli, nao watatikisika kama unyasi unavyotikiswa mtoni. Atawang'oa kutoka nchi hii nzuri aliyowapa babu zao, na kuwatawanya mbali, ng'ambo ya mto Eufrate, kwa sababu wamemkasirisha Mwenyezi-Mungu kwa kujitengenezea sanamu za Ashera, mungu wa kike.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye BWANA ataipiga Israeli, hata iwe kama unyasi unaosukwasukwa juu ya maji. Ataing'oa Israeli kutoka nchi hii nzuri aliyowapa baba zao na kuwatawanya ng'ambo ya Mto Eufrati, kwa sababu wamemghadhibisha BWANA kwa kutengeneza nguzo za Ashera.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye bwana ataipiga Israeli, hata iwe kama unyasi unaosukwasukwa juu ya maji. Ataing’oa Israeli kutoka nchi hii nzuri aliyowapa baba zao na kuwatawanya ng’ambo ya Mto Frati, kwa sababu wamemghadhibisha bwana kwa kutengeneza nguzo za Ashera
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa BWANA atawapiga Israeli kama manyasi yatikiswavyo majini; naye atawang'oa Israeli katika nchi hii njema, aliyowapa baba zao, naye atawatawanya ng'ambo ya Mto; kwa sababu wamejitengenezea Maashera yao, wakimkasirisha BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naam, tangu sasa, Mwenyezi-Mungu atawapiga watu wa Israeli, nao watatikisika kama unyasi unavyotikiswa mtoni. Atawangoa kutoka nchi hii nzuri aliyowapa babu zao, na kuwatawanya mbali, ngambo ya mto Eufrate, kwa sababu wamemkasirisha Mwenyezi-Mungu kwa kujitengenezea sanamu za Ashera, mungu wa kike.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Bwana atakapowapiga Waisiraeli, kama matete yanavyotikiswa majini; atawang'oa Waisiraeli katika nchi hii njema, aliyowapa baba zao, awatawanye ng'ambo ya lile jito kubwa, kwa kuwa wamejitengenezea miti ya Ashera inayomkasirisha Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa BWANA atawapiga Israeli kama manyasi yatikiswavyo majini; naye atawang’oa Israeli katika nchi hii njema, aliyowapa baba zao, naye atawatawanya ng’ambo ya Mto; kwa sababu wamejifanyia maashera yao, wakimkasirisha BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hakika, tangu sasa, Yawe atawapiga watu wa Israeli, nao watatikisika kama unyasi unavyotikiswa ndani ya muto. Atawaongoa kutoka inchi hii nzuri aliyowapa babu zao, na kuwatawanya mbali, ngambo ya muto Furati, kwa sababu wamemukasirikisha Yawe kwa kujitengenezea sanamu za Ashera.